Cristiano Ronaldo ameomba radhi kwa kufunga goli muhimu ambalo limewaondosha Manchester United katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya huku akisema alisumbuliwa namna alivyokuwa alichukuliwa na mazingira ya dimba lake la nyumbani la zamani la Old Trafford usiku wa jana.
Nyota huyo wa soka mwenye thamani kubwa ulimwenguni aliyeondoka Manchester na kuelekea Madrid kwa thamani ya pauni milioni £80 mwaka 2009 usiku wa jana alifunga goli safi la jitihada binafsi akitereza kuuwahi mpira wa krosi kunako dakika ya 69 licha ya kwamba uwezo ndani ya mchezo huo ulikuwa chini.
Ronaldo
alikuwa akipokea maneno ya dhihaka kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa United licha ya kwamba mashabiki wengi wa klabu hiyo walionekana kumfurahia mchezaji wao huyo wa zamani.
Cristiano Ronaldo anaonekana mwenye huzuni wakati yeye na wachezaji wenzake wa Real Madrid wakiondoka uwanjani usiku wa jana.
Akiongea na gazeti la Marca, Ronaldo amenukuliwa akisema 'samahanini Manchester United lakini nimefanya kazi yangu lakini naifurahia timu nzima.'
Pia amekubali juu ya namna alivyokuwa anga la Old Trafford lilivyokuwa likimchulia usiku wa jana na kuongeza kuwa
'kwa mara ya kwanza katika soka nilijikuta nikiadhibiwa na mazingira. Sikuwa vizuri, walikuwa wengi wenye hisia mbalimbali juu yangu.'
No comments:
Post a Comment