Jose Mourinho huenda akarejea Chelsea majira ya kiangazi. |
Kocha Real Madrid Jose Mourinho amedokeza juu ya uwezakano wa kurudi kwake katika moja klabu zake za zamani akidai kuwa huenda karudi katika moja ya vilabu ambavyo aliwahi kuvifundisha huko nyuma.
Hatma ya baadaye ya kocha huyo raia wa Ureno imekuwa katika mashaka makubwa licha ya kufanikiwa kulitwaa taji la ligi kuu nchini Hispania 'Primera Division' na sasa wakiendelea kuwa vizuri katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya.
Mourinho alitwaa mataji mawili katika ligi kuu ya nchini England 'Premier League' akiwa na klabu ya Chelsea kabla ya kuihama klabu hiyo mwaka 2007 na mara kadhaa amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea katika viunga vya Stamford Bridge kuchuakua nafasi ya meneja wa muda Rafael Benitez.
Bosi huyo wa zamani wa Porto, Chelsea na Inter Milan amenukuliwa akisema
'Nimekuwa katika hali sintofahamu na sijui nini kitatokea katika msimu wa ujao.
Mourinho anatarajiwa kuondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu.
'Si rahisi kuamua mwelekeo mpya baada ya kufanya kazi nchini England, Ureno, Italia na Hispania. Pengine naweza kurejea sehemu niliyokuwepo hapo kabla. Subiri surprises.'
No comments:
Post a Comment