Thomas Ulimwengu katikati akipongezwa na wachezaji wenzake wa Stars baada ya kuandika bao la tatu dhidi ya Morroco. |
Shomari Kapombe akidhibitiwa kwa kuvutwa jezi na mchezji wa Morocco angalia picha kwa uzuri. |
Super Samatta 'Sama boy' akiwaburuza waarabu wa Morroco uwanja wa taifa hapo jana. |
TIMU ya Taifa "Taifa Stars" leo imeiibwaga Morocco mabao 3-1 katika
mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia
mwakani nchini Brazil.
Washambuliaji wawili wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waliofunga mabao
hayo.
Samatta alifunga mawili na Ulimwengu aliyetokea benchi dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto alifunga moja.
Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C
kwa pointi sita, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kwa pointi saba,
baada ya jana kushinda 3-0 dhidi ya Gambia.
Kipindi cha pili, Stars walianza na mabadiliko, kocha Kim Poulsen
akimtoa Kazimoto na kumuingiza Ulimwengu aliyekwenda kubadilisha
mchezo.
Katika dakika ya 46, mpira wa kwanza kuugusa Thomas Ulimwengu ambao
alirushiwa na beki Erasto Nyoni aliunganisha nyavuni na kuipatia Stars
bao la kwanza.
Bao hilo liliongeza kasi ya mchezo kwa upande wa Stars na katika dakika
ya 67, Samatta alifunga bao la pili akimchambua kipa Nadir Lamyaghri
baada ya kupokea pasi ya Ulimwengu na kuifanya Morocco kuchanganyikiwa
baada ya bao la pili na kuruhusu Stars kutawala zaidi mchezo.
Kama vile siyo Stars walikuwa wanapiga pasi zisizo na idadi na kuwapa
burudani mashabiki wa soka wa Tanzania waliyokuwa waliokuwa wamejaa
uwanja bila kujali mvua iliyonyesha mchana na kusababisha mafuriko
sehemu kadhaa za jiji la Da r es Salaam
Kazi nzuri ya Ulimwengu aliyepambana na beki wa Morocco na kumzidi nguvu
hatimaye kufanikiwa kupiga krosi, iliyoipatia Stars bao la tatu
lililozamishwa kimiani na Samatta dakika ya 80.
Beki Abderrahim Achchakir alipewa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha chafu
refa baada ya Stars kufunga bao la tatu. Beki huyo alikuwa kama
analalamika kuchezewa rafu na Ulimwengu wakati akipiga krosi ya bao.
Baada ya bao la tatu wachezaji wa Stars walionyesha burudani kwa
kugongeana pasi nyingi hata hivyo kosa kidogo la safu ya ulinzi liliipa
nafasi Morocco kupata bao lililofungwa na Yousef Elarabi aliyetokea
benchi.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Tanzania, Kim Poulsen alisema kwamba
amefurahia matokeo na anawapongeza vijana, lakini bado ana kazi ngumu
katika mechi tatu zijazo dhidi ya Morocco na Gambia ugenini na Ivory
Coast nyumbani.
Naye kocha wa Morocco, Rachid Taoussi pamoja na kujutia nafasi nyingi
walizopoteza, alisema matokeo hayo yamemsikitisha kwani yanawaweka
katika wakati mgumu kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, alisema yamechangiwa na kuwa na timu mpya ya wachezaji
chipukizi, lakini watajipanga zaidi kwa mechi zilizobaki wafanye vizuri
na kufufua matumaini.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto
Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar
‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk 63, Frank Domayo,
Mbwana Samatta/John Bocco dk 91, Mwinyi Kazimoto/Thomas Ulimwengu dk46
na Amri Kiemba.
Morocco; Nadir Lamyaghri, Younes Belakhadr, Abdelilah Hafidi/Nuredenne
Amrabat, Zakarya Bergdich, Abderrahim Achchakir, Younes Hammal,
Abdelaziz Barrada, Issam Eladoua, Kamal Chafni, Chahir
Belghazouani/Youssef El Arabi na Hamza Abourazouk.

No comments:
Post a Comment