Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jana (Machi 24
mwaka huu) na Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh.
226,546,000.
Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 32,614
waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh.
7,000, sh.10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18
ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 34,557,864.41, maandalizi
ya mchezo sh. 28,450,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh.8,625,641.88.
Nyingine ni bonasi kwa timu ya Taifa Stars sh.
28,798,220.34, asilimia 15 ya uwanja sh. 18,917,141.01, asilimia 20 ya gharama za
mechi sh. 25,222,854.67 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) sh. 6,305,713.67.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
sh. 71,885,135.82 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 3,783,428.20 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa
TFF.
No comments:
Post a Comment