Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
ameipongeza wachezaji
wa Taifa Stars na benchi lao la ufundi,
washabiki, mdhamini na
Serikali kwa kufanikisha ushindi wa jana.
Tenga amesema ushindi
huo umetokana na ushirikiano kutoka kwa wadau
wote, na hasa wachezaji
walioonesha kiwango kikubwa kulinganisha na mechi zilizopita
ikiwemo kiwango cha kujituma uwanjani.
Amesema Serikali ni
mdau mkubwa wa mpira wa miguu katika miundombinu, usalama na idara zake
mbalimbali ikiwemo Uhamiaji ambayo imefanikisha kwa kiasi kikubwa
kuwepo kwa mechi hiyo ambapo Taifa Stars iliifunga Morocco mabao 3-1.
Katika hatua nyingine.
TENGA KUFUNGUA SEMINA
ELEKEZI COPA COCA COLA
Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
atakuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi wa semina elekezi ya michuano ya
Copa Coca Cola
itakayofanyika kesho (Machi 26 mwaka huu).
Semina hiyo
inayoshirikisha makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu
mikoa ya Tanzania Bara
na Zanzibar itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na itafunguliwa
na Rais Tenga kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
Washiriki wengine
katika semina hiyo itakayokuwa na watoa mada kutoka
TFF na wadhamini
kampuni ya Coca Cola ni waratibu wa michuano ya Umoja
wa Michezo wa Shule za
Sekondari Tanzania (UMISSETA).
No comments:
Post a Comment