Mkutano Mkuu wa Dharura
ulioitishwa na wanachama wa Simba, Machi 17
mwaka huu na kuuondoa
uongozi wa klabu hiyo si halali kwa vile
haukufuata taratibu, na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
halitambui Kamati za
Muda.
Uamuzi huo umefikiwa na
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana (Machi 24 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti
wake Alex Mgongolwa.
Kamati imebaini kuwa
kwa mujibu wa Ibara ya 22(2) ya Katiba ya Simba,
Mkutano Mkuu wa Dharura
unaitishwa na Kamati ya Utendaji baada ya
wanachama wasiopungua
500 kuwasilisha ombi hilo kwa maandishi na
kujiorodhesha. Mkutano
huo haukuitishwa na Kamati ya Utendaji ya
Simba.
Utaratibu huo
haukufuatwa ambapo barua ya Mkutano huo iliandikwa kwa
Msajili wa Klabu na
Vyama vya Michezo badala ya Kamati ya Utendaji ya
Simba ambayo ndiyo
matakwa ya Katiba ya Simba.
Kwa mujibu wa Katiba ya
Simba, Kamati ya Utendaji ndiyo inayoitisha
Mkutano Mkuu wa Dharura
baada ya kuhakiki uhai na uhalali wa wanachama
waliojiorodhesha kuomba
mkutano huo.
Kamati imesisitiza kuwa
Katiba za wanachama wote wa TFF hazina
kipengele cha kura ya
kutokuwa na imani na uongozi (vote of no
confidence), ndiyo
maana uko nyuma wanachama wa Yanga, Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa
Shinyanga (SHIREFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Tabora (TAREFA) walipiga
kura hiyo, na TFF kutotambua uamuzi wao.
Hata Katiba ya Simba
haitoi mamlaka kwa Mkutano Mkuu wa Dharura
kufukuza uongozi
uliochaguliwa.
Katiba za wanachama
wote wa TFF zimezingatia katiba mfano za
Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA) ambazo zinasema
kiongozi ataingia
madarakani kwa uchaguzi, na si kuteuliwa (Kamati ya
Muda).
Pia Kamati imesema
endapo wanachama wa Simba wangefuata taratibu na
uongozi ukakataa
kuitisha mkutano, wanachama wangetuma ombi hilo TFF
kupitia Kamati ya
Sheria ili kutoa mwongozo kwa uongozi wa Simba .
TFF ina mamlaka ya
kutoa adhabu kwa viongozi wa wanachama wake
wanaokwenda kinyume cha
Katiba zao. Pia Kamati imesisitiza kwa
wanachama wa TFF
kuitisha mikutano yao kwa mujibu wa taratibu na
Katiba zao, na wale
ambao muda umefika wafanye hivyo haraka.
No comments:
Post a Comment