WABUNGE WA MABUNGE YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NAO WAANZA CHALENJI YAO NAIROBI.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth Natongo Zziwa akifungua
rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa wabunge wa mabunge ya
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya ambayo hafanyika
kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda, Bunrundi,
Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi
haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo
jijini Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote
ambao wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.
Kikosi cha Uganda: Baada ya uzinduzi timu ya Bunge la Uganda na timu ya
Bunge la Afrika Mashariki ndizo zilizofungua dimba ambapo zilitoka sare
ya bao moja kwa moja. Mechi itakayofuata ni kati ya Tanzania na Kenya.
Kikosi cha Tanzania kikiusoma mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment