Kilimanjaro
Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala,
inarejea Dar es Salaam leo Jumapili jioni (Desemba 9, 2012).
Timu hiyo itatua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili
jioni kwa ndege ya PrecisionAir.
Baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza
kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba 10, 2012) saa 6 kamili
mchana ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza
kikosi chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar
es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika,
Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa
Taifa.
No comments:
Post a Comment