BONANZA LA MIAKA 51 YA UHURU VIWANJA VYA GYMKHANA KATIKA PICHA.
|
Mbozi Katala wa TASWA FC na Pastory wa NMB wakipambana kwenye mchezo wa awali, hata hivyo walitoka sare ya 1-1 |
|
Azam Group |
|
Gymkhana FC
Bonanza la kusheherekea miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika limefanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo.
Bonanza hilo
liliandaliwa na kampuni ya Vennedrick (T) Limited kupitia Mkurugenzi
wake Fredrick Mwakalebela na kudhaminiwa na NMB banki.
Bonanza hilo liliendeshwa kwa mtindo wa ligi na timu mbili toka kila kundi zikafuzu hatua ya nusu fainali na hatimaye fainali.
Timu za Barrick, NMB, DSTV na Radio Times zilikuwa katika kundi A na TASWA FC, Jubilee, Azam Group na wenyeji Gymkhana walikuwa katika kundi B
Wenyeji Gymkana waliibuka washindi na kukabidhiwa kikombe huku Times fm ikitajwa kuwa timu yenye nidhamu.
Hata hivyo katika hatua ya nusu fainali kuliibuka vurugu za hapa na pale katika michezo yote miwili.
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment