Makamu wa Rais wa Uganda Ssekandi akimkabidhi kombe nahodha wa Uganda cranes Hassan Waswa taji cha chalenji baada ya kuichapa Harambee Stars kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uwanja wa Namboole. |
Wachezaji wa Uganda Cranes katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kombe la chalenji 2012 pamoja na hundi ya mfano yenye thamani za dolari za kimarekani 30,000. |
Uganda
Cranes ilianza kuandika bao la kuongoza kunako dakika ya 27 katika kipindi cha
kwanza kupitia Anthony Kimani likiwa ni goli la kujifunga baada ya mpira
uliopigwa na Robert Ssentongo kumgonga baada ya mpira wa kashikashi wa Joseph
Ochaya.
Kipindi cha
pili Kenya ilikuwa katika uwezo mzuri na kunako dakika ya 87 juhudi zao zilizaa
matunda baada ya Edwin Lavasta kuandika bao la kusawazisha baada ya kupokea
mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto.
Wakati ikidhaniwa
kuwa mchezo huo ungemalizika ndani ya dakika 90 kwa sare, Geoffrey ‘Baba’
Kizito akaifungia Uganda bao la pili na la ushindi kunako dakika ya 90.
Kiungo huyo
wa zamani wa SC Villa na Express FC aliunganishwa kwa kichwa mpira wa adhabu wa
Robert Ssentongo baada ya Abdallah Juma kuunawa mpira nje kidogo ya kisanduku
cha hatari.
Uganda
imetengeneza rekodi ya kuchukua taji hilo mara 13.
Brian Umony wa
Uganda ametajwa kuwa mchezaji bora wa michuano wakati ambapo Hamza Muwonge ametangazwa
kuwa mlinda mlango bora.
Robert
Ssentongo amepewa zawadi ya kiatu cha dhahabu licha ya kuwa na magoli machache
kwa washambuliaji wawili wa Kilimanjaro John Raphael Bocco na Mrisho Ngassa ambao
wamefunga magoli matano kila mmoja.
Mapema katika
mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Zanziba ilichapa Kilimanjaro Stars kwa mabao
6-5 kwa njia ya kimwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao
1-1
Bal la Kilimanjaro
lilifungwa na Mwinyi Kazimoto kunako dakika ya 20 huku bao la Zanzibar
likifungwa na Othman Alliy kunako dakika ya 86 ya mchezo.
Zanzibar imezawadiwa
dolari za kimarekani 10000.
Kilimanjaro: Juma Kaseja, Erasto Edward Nyoni,
Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yodan, Amri Kiemba, Athman Idd, Shaban
Musa, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Alfan Ngasa, John Rapheal Bosco
ZANZIBAR: Abdalla Rashid Abdalla, Nadir
Cannavaro, Nassor Masoud Said, Samih Nuhu Haji, Aggrey Ambrose Morris, Sabri
Alliy Makame, Suleyman Kassim Suleyman, Khamis Mcha Khamis, Jaku Juma Jaku,
Seif Rashid Abdalla, Abdulghan Gulam Abdalla.
No comments:
Post a Comment