Ripoti ya uchunguzi kwamba iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi iliendesha
mipango ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika miaka
ya 1970, ikiungwa mkono na serikali, imechapishwa.
Mradi uliofadhiliwa na serikali wa dawa za kuongeza nguvu mwilini pia
ulitumiwa katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki, lakini ripoti ya
utafiti uliofanywa na jopo kutoka chuo kimoja kikuu mjini Berlin pia
imesema kiwango cha matumizi ya dawa hizo kilikuwa cha kutisha katika
iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki.
Kwa kuzingatia mahojiano yaliyofanywa na zaidi ya mashahidi 50, timu
kutoka chuo kikuu cha Humboldt kilitumia miaka mitatu kufanya utafiti wa
ripoti yenye kurasa 800 uliopewa kichwa “matumizi ya dawa za kuongeza
nguvu mwilini nchini Ujerumani kuanzia mwaka wa 1950 hadi leo”.
Ripoti hiyo inadai kuwa baadhi ya wanasiasa wa wakati huo walijua kuhusu
mpango huo na kuna shahidi mmoja aliyesema kuwa waziri mmoja wa mambo ya
ndani ambaye hajatajwa jina lake alisema kuwa “wanariadha wao wa
iliyokuwa Ujerumani ya magharibi walistahili kuwa na mazingira sawa ya
kabla ya ushindani na wenzao wa mashariki.”
Huyu hapa waziri wa zamani wa mambo ya ndani Gerhard Groß anasema "Kile
ambacho kimesababisha nchi nyingine kupata mafanikio katika mazoezi na
mashindano ya kimataifa, kimewanyima wachezaji wetu fursa".
Ripoti hiyo haijachapishwa, lakini sehemu ya utafiti huo kuanzia mwaka
wa 2012, imechapishwa na gazeti moja la Ujerumani suddeutsche zeitung
ambalo lilifichua Jumamosi kuwa matumizi ya dawa hizo yalifanywa katika
vitengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na riadha na mpira wa miguu yaani kabumbu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Christoph Bergner anasema matokeo
ya mwisho yanastahili kupitiwa kabla ya kuchapishwa. Anasema "wizara ya
mambo ya ndani ya Ujerumani haijapinga kufanya uchunguzi kuhusu suala
hilo.
Tumekuwa tukiunga mkono taasisi ya michezo na sayansi kwamba
mahitaji ya kuzuia utoaji wa data lazima ulindwe.
No comments:
Post a Comment