Taarifa zinasema
kuwa Gervinho na Marouane Chamakh wanakaribia kukamilisha uhamisho wao wa
kuondoka katika klabu yao ya Arsenal, hii ikiwa ni kwa mujibu wa meneja wa
washika bunduki Arsene Wenger.
Mshambuliaji
wa kimataifawa Ivory Coast Gervinho, ambaye alijiunga na washika mitutu hao kwa
ada ya uhamisho ya pauni milioni £11 akitokea Lille mwaka 2011, aliwasili nchini
Italia Jumapili kumalizia mipango yake ya kujiunga na ligi ya nchi hiyo inayojulikana kama Serie A katika klabu
ya Roma kwa ada iliyoripotiwa kuwa ni pauni milioni £6.9.
Kwa upande
wake Chamakh, ambaye alihamia klabu hiyo akitokea katika klabu ya Bordeaux mwaka
2010, anajipanga na kujiunga na Crystal Palace, licha ya kwamba bado
haijaamuliwa endapo uhamisho wake utakuwa ni wa mkopo au wa minajili ya kudumu.
Wote
wamekuwa lawamani ndani ya klabu hiyo kutoka pande za London ya kaskazini kwa
kutokuwa katika ubora wa kuwepo katika kikosi cha kwanza.
Gervinho
mwenye umri wa miaka 26, alifunga jumla ya magoli 11 katika jumla ya michezo 63
atakuwa akijiunga na bosi wa Roma Rudi Garcia, ambaye alikuwa naye katika klabu
ya Lille.
Baada ya
kuichezea West Ham kwa mkopo msimu uliopita ,Chamakh alishindwa kushawishi
kurejea kwa washika mitutu na sasa
safari yake ikiwa ni Palace ambao anaonekana kama ndiye mwenye thamani ya juu
katika usajili wa klabu hiyo majira ya kiangazi.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 29 alifunga jumla ya magoli 11 katika msimu wa kwanza
ndani ya Arsenal lakini alishindwa kuendeleza ubora wake ndani ya klabu hiyo
baadaye.
Kikosi cha
mzee Wenger kilibanjuliwa mabao 2-1 na Galatasaray Jumapili huku mshambuliaji
wa zamani wa Chelsea Didier Drogba akifunga magoli yote huku kikosi hicho kikitokea
nyuma kimatokeo.
Mpaka sasa
Arsenal imefanikiwa kufanya usajili wa mchezaji mmoja tu mwenye umri wa miaka 20
raia wa Ufaransa mshambuliaji Yaya Sanogo kwa uhamisho huru akitokea Auxerre.
Wayne Rooney: Manchester United
yakataa ombi la pili la Chelsea kumtaka Rooney.
Manchester
United imeitupia mbalia ofa kutoka katika klabu ya Chelsea kwa ajili ya
mshambuliaji wa kimataifa wa England Wayne Rooney.
Ombi hilo
lilifanywa usiku wa jana ambayo ilikuwa na thamani ya pauni milioni £25 lakini United
imeendelea kung’ang’ania msimamo wake kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 27 hauzwi.
Rooney, ambaye
amekuwa akiendelea kutaka kuondoka United, aliameachwa kueleka katika mchezo wa kesho usiku Jumanne katika safari
ya michezo ya kujiandaa na msimu huko Stockholm akiarifiwa kuwa ana matatizo ya
bega.
Imefahamika
kuwa mshambuliaji huyo alipatwa na dharuba wakati wa mchezo usiokuwa na
mashabiki dhidi ya Real Betis Jumamosi.
Chelsea ilianza
kuweka ombi la kumtaka Rooney kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £20 ambayo
ilipigwa chini mwezi uliopita wamerejea tena na ombi la pili kwa kuongeza dau
lao.
Meneja wa United
David Moyes ameendelea kusisitiza kuwa Rooney atasalia kwa mabingwa hao wa England
huku meneja wa Chelsea Jose Mourinho akiendelea kudhania kumpeleka darajani Stamford.
Luis Suarez: Brendan Rodgers anasema Arsenal wanacheza ngoma ya kujifurahisha kuhusu Suarez
Bosi wa Liverpool
Brendan Rodgers anasema klabu ya Arsenal ni kama inajifurahisha katika jaribio
lao la kutaka kumsajili mshambuliaji wake Luis Suarez.
Liverpool imeipiga
chini ofa ya rekodi ya Arsenal ya pauni milioni £40 na ziada ya pauni milioni £1, jumla yake ambao inaonekana ni kama itawezesha
kuvunja mkataba wa Suarez.
Liverpool inasema
ofa ya Arsenal kwa mshambuliaji huyo ni ya chini kwa mshambuliaji huyo mwenye
umri wa miaka 26.
Suarez
ambaye alifunga jumla ya magoli 30 msimu uliopita alijiunga na wekundu hao
mwaka 2011 akitokea Ajax kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £22.7 na ana
mkataba wa nyongeza alioingia na klabu yake Agosti 2012.
Liverpool pia
imefanya maombi mengine ikiwa ni pamoja na kumtaka mshambuliaji wa
Atletico Madrid Diego Costa kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £21 pamoja na
hayo bado Rodgers ameendelea kusisitiza kuwa hana nia ya kumuuza Suarez.
No comments:
Post a Comment