Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi
wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye
umri sahihi katika michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola 2013.
Ametoa mwito
huo leo (Machi 26 mwaka huu) wakati akifungua semina elekezi ya michuano ya
Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri
chini ya miaka 15.
Rais Tenga
amesema hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri
unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na
kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu.
“Kwanza nawashukuru kwa kutenga muda wenu na
kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye
mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta
mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya yale
tutakayokubaliana,” amesema Tenga.
Pia
ameishukuru kampuni ya Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano hiyo tangu
mwaka 2007 ambapo semina hiyo elekezi inayoshirikisha makatibu wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ni ya saba
mfululizo.
Ratiba ya michuano hiyo kuanzia mwaka huu
imebadilika ambapo sasa itaanzia ngazi ya wilaya Aprili wakati fainali katika
ngazi ya Taifa itachezwa Septemba.
No comments:
Post a Comment