Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea kesho (Machi 27 mwaka huu)
kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa mgeni ya Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja huo
wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenye
ushindi kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.
Mechi
nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam
kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Azam inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kukusanya alama itakuwa ikihitaji ushindi kwa hali na mali ikiwa ni kwa lengo kuendeleza mbio za kuwania taji kwa kupunguza mwanya wa alama baina yake na vinara hao.
No comments:
Post a Comment