Klabu ya Reading
ya nchini England imemtangaza bosi wa zamani wa Southampton Nigel Adkins kuwa
meneja wake mpya.
Adkins,
ambaye anachukua nafasi ya Brian McDermott, amesaini mkataba wa miaka mitatu na
nusu ambao utamuweka ndani ya viunga vya Madejski mpaka kiangazi 2016.
Akiongea
baada ya kusaini mkataba huo Adkins, ambaye atakuwa akisaidiwa na Andy Crosby,
amesema kuwa Reading iko katika ligi kuu ya nchini England na kwamba kibarua
chake ni kuhakikisha klabu hiyo inasalia katika ligi hiyo na kwamba
amefurahishwa na kupata kazi hiyo.
Mtangulizi
wake McDermott alitupiwa virago machi 11 na klabu hiyo baada ya kupata matokeo
mabaya ya vichapo vinne mfululizo na kuiweka timu hiyo katika nafasi ya hatari
ya kushuka daraja .
Mmiliki wa
Readind Anton Zingarevich amenukuliwa akisema kuwa amefurahishwa na kumpata Nigel
kwasababu anaamini ni chaguo sahihi kwa klabu hiyo.
Mtihani wake
wa kwanza utakuwa ni Jumamosi hii dhidi ya Arsenal kabla ya kuungana tena na
kikosi chake cha zamani Southampton Aprili 6 pale ambapo klabu hiyo itakapo
ifuata Reading ukiwa ni mchezo ambao utakuwa ukiwakutanisha vibonde hao wa
msimamo wa ligi ya England.
Serikali ya Misri yaruhusu 10,000
kushuhudia mchezo dhidi ya Zimbabwe.
Takribani
mshabiki elfu kumi nchini Misri wanajiopanga kuishangilia timu ya taifa ya
Misri itakapo kuwa uwanjani kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe Jumanne ijayo
ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2014.
Wizara ya
mambo ya ndani ya Misri imetangaza kuruhusu idadi hiyo ya mashabiki kuingia
uwanjani kuwashangilia Mafarao kwa mara ya kwanza ndani ya ardhi ya nchi hiyo,
tangu kuwekwa kwa marufuku iliyotokana na maafa ya februari 2012 katika uwanja
wa Port Said, ambapo jumla ya mashabiki 70 walipoteza maisha.
Vurugu hizo
zilitokea wakati wa mchezo baina ya Al Masry na Al Ahly ambapo hivi karibuni hukumu
ya kifo ilitolewa kwa mashabiki kadhaa waliopatinaka
na hatia ya kusababisha kuvugu hizo.
Misri
inaamini kuwa uwepo wa mashabiki hao uwanjani kutaongeza hamasa ya kikosi chao
cha timu ya taifa kuweza kufanya vizuri na hatimaye kufuzu fainali zijazo za
kombe la dunia mwaka 2014 zitakazo fanyika nchini Brazil na kurejesha nyuma
kumbukumbu ya mafanikio yao ya mwaka 1990.
Ushindi
dhidi ya Zimbabwe unatazamwa kama mwanzo mzuri kwa Misri kuingia raundi ya pili
ya hatua ya mtoano kwani watatengeneza mwanya wa alama tano mbele ya Guinea, ambapo
kinara pekee wa kundi atakuwa anasonga mbele kwenye hatua hiyo.
Zimbabwe itakuwa
ikiongozwa kwa mara ya kwanza na kocha wa kijerumani Klaus-Dieter Pagels katika
michezo ya kimashindano.
TONY ANASEMA
ALIMSHAURI PEP GUARDIAOLA KUJIUNGA MUNICH.
Luca Toni
ametanabaisha kuwa bosi mtarajiwa wa Bayern Munich Pep Guardiola amefanya naye
mazungumzo kwa njia ya simu kabla ya kuanguka saini ya kuingia mkataba wa miaka
mitatu na Bavarians.
Mshambuliaji
huyo wa Fiorentina na kocha wa zamani wa Barcelona waliwahi kufanya kazi pamoja
katika klabu ya Brescia kati ya mwaka 2001 na 2003 jambo ambalo limemfanya
Guardiola kutokusita kuwasiliana na Toni na kuhitaji ushauri wake kabla ya
kuelekea Allianz Arena.
Amenukuliwa
Toni akisema,
"Alinipigia
na kuniuliza kuwa ninaonaje hali ya Munich na jinsi nilivyokuwa nikiifahamu
klabu hiyo wakati wa kipindi cha utumishi wangu"
"Bayern
ni klabu safi sana. Maamuzi yake ya kuelekea Bayern yalikuwa sahihi kwake na
klabu pia. Bayern kwasasa wana kocha bora na dunia kwa ujumla.
"Naamini
kuwa Bayern itakuwa haishikiki Ulaya ndani ya muda mfupi"
Toni aliwahi
kuvaa jezi ya Bayern kuanzia mwaka 2007 mpaka 2010, na kushinda taji moja la
Bundesliga na moja la DFB-Pokal wakati wa utumishi wake ndani ya Munich.
McClaren awakumbusha na kuwausia vijana wa Roy
Hodgson kuelekea mchezo dhidi ya Montenegro.
Bosi wa
zamani wa England Steve McClaren ameitaka timu ya taifa ya England maarufu kama
‘Three Lions’ kuonyesha kuwa wamejifunza kutokana na makosa ya miaka miwili
iliyopita yaliyotokana na Wayne Rooney ambaye alionyshwa kadi nyekundu kuelekea
kwenye mchezo dhidi ya Montenegro hii leo.
Mshambuliaji
huyo wa Manchester United atakuwa akirejea uwanja wa Podgorica City kwa
mara ya kwanza tangu alipokabidhiwa kadi hiyo alipokuwa katika dhamira ya
kutaka kumfanyia kitu mbaya Miodrag Dzuzdovic wakati timu hizo zilipokutana kwa mara ya mwishoni mwaka
2011.
McClaren amesema
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na wenzake wanapaswa kuwa makini
kujizuia na mazingira yatakayo kuwa yakiuuzunguka mchezo huo"
Ni kweli wanaweza kushinda mchezo huo bila wasiwasi lakini hili ni jaribio la uimara wao wa akili wa kupambana na mazingira ya nje ya uwanja wanapokuwa wanacheza na haya mataifa makubwa barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment