KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 27, 2013

Burns aogopa kuvuliwa ubingwa akubali kupigana na mkali alisiyepigika Gonzalez

Signed and sealed: Ricky Burns with promoter Eddie Hearn ahead of his fight in Glasgow
Ricky Burns baada ya kutia saini akiwa na mtayarishaji Eddie Hearn kuelekea pambano la Glasgow.
 Ricky Burns atatetea taji lake la ubingwa wa dunia wa WBO la uzito wa lightweight dhidi ya Jose Gonzalez katika ukumbi wa Emirates Arena mjini Glasgow May 11.

Bondia huyo raia wa Scotland hivi karibuni amekuwa nje ya ulingo tangu apambane na kumtwanga Kevin Mitchell mwezi Septemba mwaka jana.
Burns mwenye umri wa miaka 29, hapo kabla alikuwa pambane na bingwa wa IBF Miguel Vazquez mjini London.
Ricky Burns alikuwa hana chaguo lingine isipokuwa ni kukubali kukabiliana na Gonzalez kufuatia bodi ya WBO kutishia kumvua ubingwa wake kama atataka kupata mwelekeo mwingine.

 Bodi ya utawala ya WBO iliweka muda wa mwisho wa bondia huyo kupokonywa ubingwa huo kuwa ni usiku wa juzi ambapo Eddie Hearn na promota wa Gonzalez, Peter Rivera wakalazimika kukubali kucheza mchezo huo.
amenukuliwa Burns akisema 
'kwasasa ninacho kiangalia ni namna ya kuelekea kwenye pambano hilo la May 11,'

 'Gonzalez ni bondia mwenye ngumi nzuri na rekodi nzuri ya KO, lakini nimepigana na mabondia wengi wazuri huko nyuma hivyo hiyo hainitishi'
Gonzalez mwenye umri wa miaka 29, ameshinda mapambano 22 ya kiushindani ambapo ameshinda mapambano 17.
Scottish invasion: The card in May will feature a stack of fighters from north of the border

No comments:

Post a Comment