KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 27, 2013

LUIS SUAREZ KWA MARA NYINGINE AMTWANGA MTU NGUMI YA USONI. HUYU NI MLINZI JARA GONZALO WA CHILE.

Take that: Luis Suarez hits Gonzalo Jara while the pair tussle at a corner
Pichani Luis Suarez akionekana anamtwanga ngumi Gonzalo Jara wakati wakisubiri mpira wa kona kupigwa.
Luis Suarez umefanya tena vitu vyake usiku wa jana baada ya kumchapa ngumi ya uso mlinzi wa timu ya taifa ya Chile Gonzalo Jara wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo alifanya kitendo hicho wakati wakishikana kuelekea kupigwa kwa mpira wa kona na hivyo alishindwa kuvumilia ghasia za kukabwa na mlinzi huyo na hivyo kuamua kumtwanga ngumi akitumia mkono wake wa kulia.
Jara alishindwa kuvumilia na kuanza kutupiana maneno ya hapa na pale bila ya kuwepo hali ya kushikana.
Wakati tukio hilo likitokea tayari Chile walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 lililokuwa limefungwa na Esteban Paredes.

Dakika 90 za mchezo huo zilishuhudia Chile ikiibwaga Uruguay kwa mabao 2-0, huku bao la pili likifungwa na Eduardo Vargas kunako dakika za lala salama za mchezo huo.

Matokeo hayo yameifanya Chile kuipiku Uruguay kwa alama mbili na kushika nafasi ya nne katika msimamo wa kundi hilo.

 Timu nne zitakazo maliza katika nafasi ya nne za juu zitakuwa zinafuzu moja kwa moja kuelekea katika fainali za kombe la dunia zikiungana na wenyeji wa mashindano Brazil na timu itakayoshika nafasi ya ikisubiri kupitia tundu la mchezo wa play off.
Msimamo wa kundi la nchi za Marekani ya kusini FIFA 2014 uko hivi.
 
South American qualifying table for the FIFA 2014 World Cup in Brazil Pain game: Suarez is usually targeted by opposition defenders
Suarez akionekana kugumia maumivu baada ya kukabiliwa vilivyo na mlinzi wa Chile.

Argentina ina ongoza kundi hilo na ikiwa katika mazingira mazuri ya kufuzu baada ya kuongoza kwa alama 24 na jana usiku ilikwenda sare na Bolivia huku nyota wake Lionel Messi akinukuliwa kulalamikia hali ya hewa ya mji wa La Paz.
Hard to breathe: Lionel Messi and Co found it tough going in La Paz
Lionel Messi na hali ya hewa ya La Paz.

Messi
Katika mchezo baina ya Argentina na Bolivia wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi lililowekwa nyavuni na Marcelo Martins kabla ya Ever Banega kuswazisha muda mfupi kabla ya mapumziko.

No comments:

Post a Comment