KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, March 27, 2013

LIGI KUU TANZANIA BARA: SIMBA NA KAGERA , AZAM NA PRISONS LEO

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea tena leo (Machi 27kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa mgeni ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
 
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenye ushindi kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.

Mechi nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Azam inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kukusanya alama itakuwa ikihitaji ushindi kwa hali na mali ikiwa ni kwa lengo kuendeleza mbio za kuwania taji kwa kupunguza mwanya wa alama baina yake na vinara hao.

No comments:

Post a Comment