Msimu mpya wa ligi ya soka Ujerumani umeng'oa nanga mwishoni mwa juma
kwa mechi za duru ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Ujerumani na kama
kawaida dimba hilo halikukosa mshangao.
Werder Bremen na Borussia Moenchengladbach walikuwa waathiriwa wa kwanza
wa Bundesliga kubanduliwa nje ya kombe hilo kufikia sasa na timu za
ligi ya daraja ya tatu.
Kocha Robin Dutt wa Werder Bremen hakuamini macho yake baada ya kuzidiwa nguvu.
Timu nyingine mbili za Bundesliga zilitolewa wakatin klabu
iliyopandishwa msimu huu Eintracht Braunschweig ilipofungwa magoli
mawili kwa moja na timu ya daraja ya pili Arminia Bielefeld, nayo
Nuremberg ikashindwa kupitia mikwaju ya penalty mabao matano kwa manne
na klabu ya daraja ya pili Sandhausen.
Bremen walitemwa nje kwa kufungwa mabao matatu wka moja katika muda wa
nyongeza na klabu ya Saarbrücken ikiwa ni mara yao ya tatu mfululizo
kuondolewa katika dimba hilo kwenye duru ya kwanza na timu ya ligi xya
daraja ya tatu.
Huo ulikuwa mwanzo mbaya wa ligi kwa kocha mpya Robin
Dutt aliyechukua mikoba kutoka kwa Thomas Schaaf.
Nao Gladbach
walimaliza mchezo bila kufungana na Darmstadt katika muda wa ziada na
wakanyolewa kwa penalti kwa kufungwa mabao matano kwa manne.
Timu nyingine zilizofuzu kwa awamu ijayo ni Hanover, Eintracht
Frankfurt, SV Hamburg pamoja na Borussia Dortmund. Hii leo itakuwa zamu
ya Bayern Munich na Schalke ambazo zitaingia uwanjani dhidi ya wapinzani
wa daraja ya chini.
No comments:
Post a Comment