![]() |
Barcelona wanampta Thibaut Courtois kuwa mlinda mlango namba moja. |
Barcelona imezindua mpango wa kumsajili mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois wakati wa majira ya usajili ya kiangazi.
Mlinda mlango huyo raia wa Belgium ambaye anathaminishwa kwa pesa nyingi kwasasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Atletico Madrid anatazamwa na Barcelona kama ndio mawindo yao ya kwanza kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Victor Valdes.
Chelsea
haitaki kumuuza Courtois lakini mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 21 anaonekana ni mwenye hofu ya kutokupata nafasi ya kudaka Stamford Bridge kutokana na Petr Cech kuendelea kuwa katika kiwango na kwamba mpango wa Barcelona kwake unakuwa kama majaribu makubwa ya kuelekea Nou Camp.
Barcelona tayari imefanya mawasiliano na Chelsea juu ya uwezekano wa kumpaka mlinda mlango huyo lakini Chelsea inasema inataka anagalau pauni milioni £17.
Atletico
Madrid pia inaonekana inamtaka kwa minajili ya mkataba wa kudumu lakini kiwango cha pesa 'price tag' kilichotajwa na Chelsea kinaonekana kuwatoa katika ushindani wa kupata huduma yake.
Wanaonekana kugeukia kwa mlinda mlango wa Liverpool Pepe Reina aliye kwa mkopo Napoli endapo wataqshindwa kupata Courtois.
Courtois, ambaye ameichezea timu yake ya taifa ya Belgium michezo 14 mara kadhaa amekuwa akinukuliwa akisema ataamua mustakabali wake mwezi Februari
Courtois amekuwa katika kiwango bora katika klabu ya Atletico Madrid aloko kwa mkopo
No comments:
Post a Comment