KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 25, 2013

Boxing Day Etihad Stadium baina ya City na Liverpool mambo ni kama hivi.............

Barclays Premier League

  • Venue: Etihad Stadium
  • Date: Thursday, 26 December
TEAM NEWS
Manchester City inaendelea kuikosa huduma ya mfungaji wake Sergio Aguero na walinzi Matija Nastasic, Pablo Zabaleta na Micah Richards kuelekea hapo kesho siku ya 'Boxing Day' dhidi ya Liverpool.
Stevan Jovetic alikosekana katika mchezo dhidi ya Fulham kwasababu kutokana na homa na bado kuna mashaka juu ya uwepo wake.
Mlinzi wa Liverpool Jon Flanagan yuko mashakani kutoka na maumivu ya msuli ambayo aliayapata katika mchezo dhidi ya Cardiff.
Steven Gerrard, Daniel Sturridge, Jose Enrique na Sebastian Coates wote hao ni majeruhi wa siku nyingi

Licha ya maneno na matokeo ya mashaka ya Manchester City inapokuwa ugenini na matokeo ya uwanja wa nyumbani kuwa shwari wakishinda mara nane na kufunga magoli 35 ni rekodi inayo wapa kiburi.

Head-to-head
  • mara sita katika mara tisa walizo kutana ndani ya Premier League wamekwenda sare, huku City wakishinda mara mbili na Liverpool wakishinda 3-0 nyumbani ukiwa ni ushindi wakujivunia.
Manchester City
  • City ndio timu pekee katika ligi ya Premier ikiwa bado kupoteza alama katika uwanja wake wa nyumbani msimu huu. 
  • Idadi kubwa ya magoli 35 katika michezo nane ya kuanza msimu huu ni ya kiwango cha juu kabisa katika kipindi cha miaka 51 tangu mara ya mwisho kufanywa hivyo na Tottenham msimu wa mwaka 1962-63.
  • Wameshindwa kufunga katika siku za Boxing Day mbili zilizopita, ambapo walikwenda suluhu 0-0 dhidi ya West Brom mwaka 2011 na kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Sunderland mwaka jana.
  • Liverpool imeshinda michezo minne ya mwisho akifunga magoli 17. Kwa mara ya mwisho kufunga mfululizo michezo mitano ilikuwa ni kipindi cha mwezi April-May mwaka  2009.
  • Pia imeshinda mchezo mmoja katika michezo mitano katika kiwanja cha ugenini huku ikienda sare mara mbili na kufungwa mara mbili(D2, L2).
  • Boxing day yao ya mwisho kushinda ilikuwa 2009 walipoichapa Wolves  2-0.

No comments:

Post a Comment