Mark Kiptoo ameimarisha ushindi wake katika mashindano ya mbio za Frankfurt mwaka huu baada ya kuibuka mshindi.
Kiptoo
mbaye alimaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita aliwaongoza
wanariadha wengine wa Kenya kushinda nafasi tatu bora katika mbio za
wanaume.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye alishinda
medali ya shaba katika mbio za mita 5000 katika mashindano ya jumuiya
ya madola ,alimaliza mbio hizo na saa 2,dakika 6 na sekunde 49,katika
mbio za kusisimua ambazo ziliamuliwa ikiwa imesalia kilomita moja.
Mike
Kigen alimaliza katika nafasi ya pili kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 59
naye Gilbert Yegon akawa wa tatu kwa saa 2 dakika 7 na sekunde 8 baada
ya bingwa mtetezi pia kutoka kenya kupoteza uongozi na kundi la kwanza
katika kituo cha kilomita 30.
No comments:
Post a Comment