Cristiano Ronaldo anaelekea pazuri zaidi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or kufuatia kutangazwa kuwa mchezaji bora wa Hispania La Liga huku pia akitajwa kuwania kwa mara nyingine tena tuzo kubwa ya mchezaji bora wa dunia Ballon d'Or ikiwa ana tetea nafasi yake ya ubora baada ya kumshinda mpinzani wake Lionel Messi katika ubora wa nchini Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Hispania hapo jana baada ya kufumania nyavu mara 31 katika Ligi ya mabingwa Ulaya.
Huenda ikawa ni pigo kwa Messi, ambaye ameshinda tuzo hizo mara moja katika miaka mitano iliyopita.
Tuzo ya Ballon d'or itatangazwa mwezi Januari.
Amepongezwa na mwenzake wa Real Madrid Gareth Bale ambaye kupitia ukurasa wake wa tweeter mbali ya Ronaldo pia amewapongeza Keylor Navas, Sergio Ramos na Luka Modric.
Tuzo zingine ni kwamba meneja Diego
Simeone ambaye ameiongoza Atletico Madrid mpaka kuchukua taji amepata tuzo ya kocha bora wa mwaka wakati ambapo Sergio Ramos akipata tuzo ya mlinzi bora.
Tuzo nyingine za La Liga ni kama ifuatavyo
LA LIGA AWARDS
Best Player Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Best Coach Diego Simeone - Atletico Madrid
Best Goalkeeper Keylor Navas - Real Madrid (formerly Levante)
Best Defender Sergio Ramos - Real Madrid
Best Defensive Midfielder Luka Modric - Real Madrid
Best Attacking Midfielder Andres Iniesta - Barcelona
Best Forward Cristiano Ronaldo - Real Madrid
Best African Player Yacine Brahimi - Granada
Best South American Player Carlos Bacca - Sevilla
Revelation Rafinha Alcantara - Barcelona (loaned to Celta in 2013-14)
Best Goal Cristiano Ronaldo (vs Valencia) - Real Madrid
Fair Play Ivan Rakitic - Barcelona (formerly Sevilla)
Wakati hayo yakiwa hivyo, Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale
ndio mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati wachezaji
wanaoshindania tuzo la mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or huku
mshambulizi matata wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa
kuhifadhi taji hiloBale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza
kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid
kunyakua kombe la kilabu bingwa duniani
Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar
Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich .
Hatahivyo
hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa
kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika
katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini
akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa
kumng’ata mlinzi wa Italy Giorgio Chiellini.
No comments:
Post a Comment