Manchester United imepiga hatua moja mbele katika harakati zao za kutaka kumsajili mshambuliaji Gareth Bale mwezi Januari baada ya Real Madrid kuripitiwa kutaka kumuweka sokoni mshambuliaji huyo.
United wanaaminiwa kumuweka Bale katika chaguo lao la kwanza wakati wa kipindi cha uhamisho cha mwaka mpya huku pia wakiwa tayari kumlipa kiasi cha pauni £300,000 kwa wiki ili muradi tu ajiunge Old Trafford.
Swali kubwa ni je Madrid kweli wanataka kumuuza ama laa, lakini taarifa nchini Hispania zinaarifu kuwa Madrid wanafurahia kufanya biashara ya mchezaji huyo.
Inaelezwa kuwa meneja Carlo Ancelotti amekubali kumpoteza Bale, kwakuwa hafikirii kumtumia tena kama mchezaji wa kikosi cha kwanza kufuatia kuvutiwa zaidi na aina ya uchezaji wa Isco.
Madrid wanataka kiasi cha pauni milioni £90 kwa ajili ya kumtoa Bale.
No comments:
Post a Comment