Mchezaji wa kilabu ya Real Madrid
Christiano Ronaldo amebashiri kwamba klabu ya Manchester United
itashinda ligi kuu ya Uingereza chini ya ukufunzi wa Louis Van Gaal.
Kulingana
na gazeti la Mirror nchini Uingereza,mchezaji huyo anaamini kwamba
kilabu hiyo aliyoichezea miaka ya 2003 hadi 2009 imefanikiwa kupata
meneja mwenye uwezo kuiweka timu hiyo katika kiwango ilichowekwa
naaliyekuwa kocha wake Sir Alex Ferguson.
CR7 kama anavyojulikana
na wengi amesema kuwa Ijapokuwa Kilabu ya Chelsea chini ya Ukufunzi wa
Jose Mourinho itamaliza katika nafasi ya kwanza msimu huu,Kocha Van Gaal
atafufua matumaini ya Manchester United.
''Van Gaal ni kocha
mzuri ambaye ataifanya Manchester United kuwa bingwa tena na kama si
mwaka huu basi mwaka mmoja kutoka sasa'',alisema Ronaldo.
No comments:
Post a Comment