Manchester United wako katika maendeleo mazuri ya mazungumzo yao na mlinzi wa pembeni wa Barcelona Dani Alves wakati huu ambapo mlinzi huyo akiwa anakaribia kujiunga na Old Trafford.
United wamekuwa mbele zaidi katika mbio za kumuwania mlinzi huyo huku vilabu vingine kadhaa vya Premier League vikisukumwa na mpango wa kumsajili Alves wakiwemo Chelsea na Liverpool baada ya Alves mwenyewe kuitaka Barcelona kumruhusu kuondoka mwaka mpya.
Taarifa zinasema mpango huo unakaribia kukamilika ambapo mashetani wekundu wakiwa katika mazungumzo ya mwisho na Alves.
Tayari Mbrazil amejiweka tayati kuelekea Old Trafford na Louis van Gaal akipambana kukamilisha mpango huo.
Alves atatoa upinzani mkubwa kwa damu changa Rafael da Silva ndani ya kikosi cha United.
No comments:
Post a Comment