![]() |
Alex Ferguson akipeana mikono na mashabiki wakati akichukua kiti karibu na sehemu ya makocha wa United pembeni yake ni Wilfried Zaha (kushoto) |
Meneja wa zamani wa Manchester United Sir
Alex Ferguson anaonekana kuendelea kuwepo karibu sana na ratiba za michezo ya klabu hiyo, ambapo hii leo ikiwa ni siku ya kufunguza zawadi za sikukuu ya Krismass yaani 'Boxing Day' akionekana dimbani katika mchezo wa klabu hiyo dhidi ya Hull City uliopigwa KC Stadium.
Fergie
ameonekana akifuatilia pambano hilo kwa ukaribu zaidi akiwa amevalia vazi la koti rasmi kabisa kwa ajili ya maafisa wa Manchester United akiwa karibu na benchi la ufundi la makocha karibu pia na wachezaji wa timu hiyo akiwemo Wilfied Zaha.
Hakuna uhakika ni namna gani David Moyes anajisikia kuwa nyuma ya mtu huyu mwasisi wa benchi la ufundi aliyestaafu kuwa nyuma yake wakati kikosi kikiwa katika nafasi ya nane katika msimamo wa ligi katika kipindi ambacho kimezoeleka United kuwa katika vita ya kupigania taji.
David Moyes akifuatiliwa na meneja mstaafu.
Alex Ferguson akiwa katika vazi rasmi la maafisa wa United karibu na benchi la ufundi ndani akiwa na tai
Baada ya kuwa nyuma kimatokeo mapema kupitia kwa James Chester (mchezaji wa zamani wa United) na David Meyler, meneja huyo pengine angekuwa katika joto la mawazo nyuma yake kuna mtangulizi wake.
Hata United ilizinduka kwa kuandika goli la kichwa kupitia kwa Chris Smalling na lingine kupitia kwa Wayne Rooney na hivyo mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa sare.
Chester
akajikuta anatoka kuwa shujaa mpaka mkosefu 'hero to zero' kufuatia kujifunga goli katika kipindi cha pili na hivyo kuhitimisha hesabu ya mabao 3-2 United ikishinda kutoka nyuma kimatokeo.
Klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford sasa imejikita katika nafasi ya sita ikiwa nyuma kwa alama sita mbele ya vinara wa ligi hiyo Liverpool ambapo ushindi katika dimba la KC Stadium ulikuwa muhimu katika kurejesha matumani ya kuingia katika changamoto ya kutetea taji.
Hiyo imekuwa ndio nafasi ya chini kabisa kukaliwa na mashetani wekundu katika kipindi cha majira ya krismass katika historia ya ligi kuu Premier
League.
Hull wakiandika bao la utangulizi kupitia kwa mchezaji wa zamani wa United James Chester (katikati)
David Meyler (katikati) akiandika bao la pili la Hull kipindi cha kwanza baada ya mpira kumgonga David De Gea
Chris Smalling akifunga goli kwanza la United kwa kichwa baada ya mpira wa kona.
Wayne Rooney akiandika bao la kusawazisha la United
James Chester akijifunga na hivyo kuwapa United ushindi wa mabao 3-2 huku Wayne Rooney akishangilia
No comments:
Post a Comment