KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, February 15, 2013

SIMBA NA SUNDERLAND KUKUTANA LONDON KUZUNGUMZIA MAHUSIANO BAINA YAO CHINI YA MRADI WA INVEST IN AFRIKA.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari leo katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi. Kubwa zaidi ni juu ya ziara ya uongozi jijini London kwa ajili ya kuweka mipango ya mahusiano baina ya Simba na Sunderland. Soma taarifa chini.
Alhaji Rage akionyesha msisitizo kwa kile anacho kiongea na waandisho wa habari katika makao makuu ya klabu Simba hii leo.
Mwenyekiti wa Simba Alhaji Ismail Aden Rage akiwa na mfadhili wao Bi Rahma Al Harous wakati wakiongea na waandishi wa habari hii leo.
Bi Rahma Al Kharouz akioongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, kubwa alikuwa akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Libolo ya Angola.
Bi Rahma akiongea na waandishi wa habari
Hii ni jezi ambayo imetambulishwa hii leo.
Mwenyekiti wa Simba Alhaji Rage na kushoto ni Bi Rahma wakionyesha jezi iliyotolewa na klabu Sunderland ikiwa ni sehemu ya mradi wa uwekezaji wa klabu hiyo barani Afrika 'Invest in Afrika' ambao Simba ni moja ya klabu ambayo itafaidika na mradi huo.
Bi Rahma akiongea na wanachama wa Simba wakati aiondoka.
Wanachama wakimsindikiza.
Hawa nao walikuwa wakipiga ngoma kumlaki Bi Rahma alipokuwepo klabuni hapo.
Rais wa klabu ya Sunderland ya nchini England Shot Elis amewaalika viongozi wa klabu bingwa nchini Simba kwenda jijini London kwa ajili kukamilisha mambo mbalimbali ya kiushirikiano baina ya klabu zao chini ya mradi wa klabu hiyo wa Invest in Afrika.
Viongozi hao wa Simba wakiwa jijini London nchini England, pia watapata fursa ya kuangalia mchezo wa ligi ya soka nchini humo 'Primier League' baina ya Sunderland na Fulham mchezo utakao fanyika tarehe 02/march/2013. 

Hato yameelezwa na mwenyekiti wa Simba Alhaji Ismail Aden Rage katika mkutano wake na waandhishi wa habari hii leo katika makao makuu ya klabu hiyo Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Rage amesema hatua hiyo imefuatia jitihada zilizofanywa na Rais Jakaya Kiwete ambaye alimtambulisha Rais huyo wa Sunderland kwa viongozi wa Simba kabla ya kukutana na mwenyekiti Aden Rage na mfadhili wa Simba mama Rahma Alharous jumatatu iliyopita na kufanya mazungumzo.

Rage amesema Rais wa Sunderland awewaahidi kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya England Simba itakuwa ikipata vifaa mbalimbali vya klabu hiyo kupitia mradi wa klabu hiyo wa uwekezaji barani Afrika, ambapo vilabu ambavyo vimekuwa vikipata vifaa hivyo chini ya mradi wa Invest in Afrika vimekuwa vikipata paund milioni tatu na kwamba hiyo itakuwa ni faida kwa klabu yake ambapo pia wamekubaliana kuwa Sunderland itakuwa ikitoa msaada wa kiufundi kiufundi kwa Simba.
 Rage ambaye pia alitumia fursa hiyo kumtambulisha mfadhili wao mpya ambaye aliifandhili safari ya Simba katika ziara yao ya mazoezi nchini Oman kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara Bi Rahma Al Harouz, amesema anaamini kwa ushirikiano ulipo sasa baina yao na Bi Rahma ambaye anatambulika kama Malkia wa nyuki, na yeye Rage akimwita mpiganaji basi watafanikisha mambo mengi yenye lengo la kuleta mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
 
Sambamba na hilo Rage amesema ndani ya mazungumzo yao yaliyokuwa chanya, wamekubalina kuwa wachezaji wawili wa Simba, Shomari Kapombe na Ramadhani Singano 'Messi' waende jijini London, mara baada ya ligi kuu kumalizika kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka katika klabu hiyo ya Sunderland.

Simba tayari imeanza kupokea vifaa kutoka klabu hiyo kongwe nchini England ambavyo vina maandishi ya utambulisho wa mradi wa uwekezaji wao barani Afrika wa 'Invest in Afrika'(Tazama picha juu).

No comments:

Post a Comment