Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans kesho siku ya jumapili itashuka dimbani kuivaa timu ya Mbeya
City FC kutoka jijini Mbeya katika muendelezo wa michezo ya mzunguko wa
pili, mechi itakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Young Africans ambayo kwa sasa inakamata nafasi ya pili kwenye
msimamo wa VPL ikiwa na pointi 32, pointi moja nyuma ya vinara
wanaongoza timu ya Azam FC huku Mbeya City wakiwa nafasi ya tatu na
pointi 31.
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake
leo asubuhi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo wa kesho ambao ni
muhimu kwa vijana wa Jangwani kupata pointi 3 na kuweza kujiweka katika
nafasi nzuri ya kurejea kileleni.
Kocha mkuu Hans Van der Pluijm
amesema wameendelea kufanyia marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza
katika mchezo uliopita dhidi ya timu ya Coastal Union na kusema anaamini
vijana wake watafanya vizuri katika mchezo wa kesho.
Kuna
mapungufu yalijitokeza katika mchezo uliopita mjini Tanga dhidi ya
Coastal, tulipata nafasi kadhaa za kufunga tukashindwa kuzitumia pia
umakini haukuwa mzuri sana, tumeendelea kufanyia marekebisho mapungufu
hayo ili tuweze kufanya vizuri.
Katika mchezo wa awali uliofanyika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwezi Septemba mwaka jana, timu hizi
zilitoka sare ya mabao 1-1 huku bao la Young Africans likifungwa na
Didier Kavumbagu.
No comments:
Post a Comment