KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 1, 2014

MBANANO WA LIGI KUU TANZANIA BARA, SIMBA YAIFUMUA JKT OLJORO 4-0, TAIFA

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao
Golikipa wa JKT Oljoro akificha mpira baada ya kuudaka
Amis Tambwe akikimbia na mpira huku Nurdin Mohamed akimkimbiza
Uhuru Seleman wa Simba  na Shaib Nayoba wa JKT Oljoro wakipambana
Kikosi cha Simba
JKT Oljoro
Makocha wa Simba Loga na Matola wakisalimiana na kocha wa JKT Oljoro Hemed Morocco kabla ya mchezo kuanza

Simba ya Dar es Salaam leo iliibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 dhidi ya Oljoro JKT katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku mchezaji wake Amis Tambwe akifunga mabao matatu peke yake na kukabidhiwa mpira.

Washindi waliandika bao la kuongoza katika dakika ya 11 kupitia kwa Jonas Mkude baada ya kupigwa kona fupi na Ramadhani Singano na kumkuta mfungaji aliuyeunganisha wavuni kwa shutu kali lililompita kipa wa Oljoro Mohamed Ally.

Singano aliambaa na mpira upande wa kulia na kumpiga chenga beki wa kushoto wa Oljoro Ally Omary na kupiga krosi iliyomkuta Amis Tambwe akiwa pekee yake aliyeukwamisha mpira wavuni katika dakika ya 23.

Tambwe tena alicheka na nyavu katika dakika ya 29 baada ya kufunga kufuatia pasi kutoka kwa Amri Kiemba katikati ya uwanja na kumpasia mfungaji aliyekimbia na mpira na kuwazidi mbio mabeki kabla ya kufunga.

Katika kipindi cha kwanza Oljoro nusura wafunge baada ya Shija Mkina alikaribia kufunga lakini akiwa ndani ya eneo la hatari alisukumwa na beki Donald Msoti lakini mwamuzi Nathani Lazaro  wa Kilimanjaro kushindwa kuwapa penati.

Amiri Omary wa Oljoro alishindwa kuipatia timu yake bao licha ya kuwa katika nafasi nzuri baada ya kubaki yeye na kipa Ivo Mapunda kufuatia krosi safi ya Paul Malipesa, alishindwa kufunga na badala yake mpira ulidakwa kirahisi na Mapunda.

Simba walianza kwa kasi kushambulia lango la wapinzani na walifanikiwa kufunga bao katika dakika ya 56 na kujihakikishia `hat trick’ akimalizia krosi ya Haruna Chanongo kutoka upande wa kulia wa uwanja huo.

Simba waliutawala zaidi mchezo huo huku Oljoro wakionekana wazi kukatishwa tama na kipigo hicho.
Mwamuzi alimkabidhi mpira Tambwe kutokana na kufunga mabao hayo matatu katika mchezo mmoja, kitendo kilichoibua shangwe kwa mashabiki. Tambwe katika zunguko wa kwanza alifunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Mgambo Shooting lakini mwamuzi wa mchezo huyo alimbania.

Kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola alisema baada ya mchezo huo kuwa, timu yake ilistahili kushinda lakini mchezo ulikuwa mgumu kwani timu zilizomkiani zinataka kujanusua.

Alisema watajipanga vizuri kuhakikisha wanaendelea na ushindi katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Naye kocha wa Oljoro JKT Hemed Morocco alisema mchezo ulikuwa mgumu kwani wachezaji wake walicheza vibaya katika kipindi cha kwanza na kusababisjha kufungwamabao matatu, na aliwapongeza Simba kucheza vizuri.
Alisema kuwa Oljoro wampe muda zaidi wa kuandaa timu kwani wachezaji wake wengi ni wageni, lakini atajitahidi kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja na inafanya vizuri msimu huu.

Timu zilikuwa:Simba:Ivo Mapunda, William Luciana, Issa Rashid,Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo,Awadhi Juma, Amri Kiemba/Said Ndemla, Amis Tambwe/Uhuru Selemani na ramadhani Singano.

Oljoro JKT:Mohamed Ali, Paul Malipesa, Ali Omari, Aziz Yusuf, Nurdin Mohamed/Shaibu Nayopa, Sabri Makame/Swaleh Idd, Babu Ally/Hamis Maulid, Jacob Masawe, Amir Omari, Shija Mkina na Majaliwa Mbaga.

No comments:

Post a Comment