KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, November 30, 2013

CECAFA CHALENJI CUP: ZANZIBAR HOI KWA WAHABESHI WA SOMALIA.

Magoli mawili ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Fasika Asfan, na Salahadin Bargicho kwa njia ya penati na lingine la tatu katika dakika za majeruhi kupitia kwa mshambuliaji Yonathan Kedebe, yameiweza kuwapa ushindi wa mabao 3-1 timu ya taifa ya Ethiopia maarufu kama 'Walya stars'  dhidi ya timu ya taifa ya Zanzibar.
Huu ulikuwa ni mchezo wa kundi A wa michuano ya chalenji ya GOtv inayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika mashariki na kati cecafa.
Mchezo huo umepigwa katika dimba la Nyayo stadium jijini Nairobi hii leo.
Ethiopia ilianza kuongoza kunako dakika tano tu za mchezo kupitia Fasika Asfan kufuatia krosi nzuri ya kujituma iliyotumwa na Yousuf Yassin Salah kupitia winga ya kulia baada ya kuwapita Khamis Bakari na Wazir Salum huku sehemu ya kuchezea mbovu ikiendelea kuwaudhi wachezaji na watazamaji ambao walikuwa wachache lakini wakishangilia kwa nguvu.
Timu ya taifa ya Zanzibar ambayo ilimpoteza mshambuliaji wake tegemeo kunako dakika ya 14 Suleiman Kassim Suleiman baada ya kukumbana na maumivu makali ya msuli ilirejea na nguvu kipindi cha pili ambapo moja kati ya shambulizi zuri walillofanya liliwawezesha kuandika bao la kufutia machozi kupitia kwa Awadh Juma Issa.
Baada ya matokeo hayo ya leo ukijumlisha na matokeo ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya wenyeji Harambee stars, Ethiopia sasa wanahitaji angalau sare katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Sudan Kusini ili kuweza kusonga mbele kwenye robo fainali.

Team Line -ups:
Ethiopia:Derete Alemu (Goal keeper), Fasika Asfan (Captain), Salahadin Bargicho, Thok James, Moges Tadese, Shimekit Gugsa, Mulualem Mesfin, Mintesnote Adane, Yousuf Yassin Salah, Mehary Mena and Manaye Fantu.
Coach: Sewenet Bishaw
Zanzibar: Abdalla Rashid Abdalla, Adeyum Saleh Ahmed, Salum Khamis Bakari, Wazir Salum Omar, Sharif Hassan Rajab, Mohammed Faki Makame, Masoud Ali Mohhd, Ali Badru Ali, Suleiman Kassim Suleiman and Awadh Juma Issa.
Coach: Salum Baus Nassor

No comments:

Post a Comment