KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 16, 2012

UCHAGUZI DRFA, SAFU YAPANGWA CHINI KWA CHINI.WAANDISHI WAJITOKEZA.


Mwenyekiti kamati ya uchaguzi DRFA Alhaji Muhidin Ndolanga
Wakati uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA ukiwa umepangwa kufanyika October 14, tayari makundi katika wagombea yameanza kuonekana ikiwa jaribio la kupanga safu ya uongozi wa soka katika mkoa huo kinara katika fitna za mchezo huo pendwa.
Nafasi zinazo tarajiwa kugombewa ni mwenyekiti ambayo kuna jumla ya wagombea watano wamejitokeza kuwania nafasi hiyo. Wanao wania nafasi hiyo ni mwenyekiti anatetea nafasi yake Amin Bakhresa, Evance Aveva, Salum Mkemi, Frank Mchaki na Juma Jabri.
Kwa upande wa nafasi ya makamu mwenyekiti inawaniwa na wagombea wawili ambao Salum Mwaking’inda na Gungulwa Tambaza.
Nafasi ya katibu wamejitokeza wagombea watatu, ambao ni Msanifu Kondo, Saidi Tuli na Hamisi Ambali.
Wanao wania nafasi ya ujumbe wamejitokeza wagombea wawili ambao ni Shafii Dauda na Muhsin Balhboo, wakati ambapo wanaowania nafasi ya ujumbe wa vilabu ni Mohamed Bhinda na Benny Kisaka.
Nusa nusa za Rockersports zimebaini kuwa tayari kumeanza kujengwa safu mpya ya uongozi ya DRFA hata kabla ya uchaguzi huo haujafika , kwani kumekuwepo na kampeni za chini kwa chini zikiendelea katika zoezi hilo huku baadhi ya wagombea wakipigwa vijembe vya waziwazi ya kuwa hawana nafasi ya kuongoza soka DRFA.
Safu iliyo katika nafasi ni mwenyekiti Aveva na makamu wake ni Gungulwa Tambaza. Katibu msanifu Kondo, mjumbe Muhsini na mjumbe wa vilabu Mohamed Bhinda.
Kwa mujibu wa ratiba ya kuelekea katika tarehe ya uchaguzi huo, leo  Septemba 16 ni siku kuweka mapingamizi na mwisho wa kamati ya uchaguzi kupokea pingamizi ni Septemba 20 saa 10 alasiri.
Hakutakuwa na ada katika kuweka pingamizi, bali pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya 11(2) ya kanuni za uchaguzi.
Ratiba hii inaonesha Septemba 26 ni fursa ya kukata rufaa iwapo maamuzi yaliyotolewa na kamati DRFA hayakurishishwa na mrufaa na hiyo itakwenda kwa kamati ya TFF.
Kampeni kwa wagombea zitaanza rasmi Oktoba 4, hadi13 ambapo Oktoba 14 itakuwa uchaguzi.
Kama ilivyo ada katika miaka ya hivi karibuni chaguzi nyingi katika vyama vya soka kumekuwa na wagombea waandishi wa habari ambao wamekuwa wakishinda nafasi wanazo wania mara hii pia waandishi wa habari watatu wamejitokeza akiwemo Benny Kisaka, Shafii Dauda na  Salum Mkemi.

No comments:

Post a Comment