KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 16, 2012

SERENGETI BOYS YAENDELEA KUFANYA VITU VYAKE NYANDA ZA JUU KUSINI.


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na kambi ya mazoezi katika mikoa ya Mbeya na Njombe ambapo leo jioni (Septemba 16 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki mjini Makambako na timu ya Manispaa.
 
Serengeti Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo imeshacheza mechi nne mkoani Mbeya. Imecheza mechi hizo dhidi ya Tanzania Prisons, Mbozi United, Mbeya City na Kombaini ya Kyela na kupoteza moja tu.
 
Baada ya mechi ya kesho (Septemba 17 mwaka huu) itacheza mechi ya mwisho mkoani Njombe dhidi ya Kombaini ya Makambako na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi dhidi ya Misri.
 
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika Machi mwakani nchini Morocco itachezwa Oktoba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment