KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 16, 2012

MAPATO JKT RUVU DHIDI YA RUVU SHOOTING AIBU,MECHI YA SIMBA, LYON YAINGIZA MIL 67/- NA YANGA NA PRISON MILION 50.

Wakati sakata la udhamini wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel kwa klabu ya Afrikan Lyon likiendelea kupendezesha vichwa vya habari na huku mjadala mpana ukionekana kuanza kuchomoza kwa wadau wa soka nchini, hali ya mambo imeanza kudhihirisha kuwa bila vilabu kupata wadhamini binafsi hali itaendelea kuwa mbaya kwa upande wa vilabu hivyo.
 
Maneno hayo yanadhihirishwa na taarifa ya shirikisho la soka nchini TFF kuhusu mapato yaliyo patikana kutokana na viingilio vya michezo saba ya ligi hiyo iliyoanza jana nchini ambapo timu 14 zinazo shiriki ligi hiyo zilijitupa viwanjani.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hali imeonekana kuwa ni ya kusikitisha katika mchezo uliochezwa kule Chamazi kati ya ndugu wawili toka jeshini, JKT Ruvu na Ruvu Shooting mchezo ambao umeingiza shilingi 340,000. 
 
Kufuatia mapato hayo mgao ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
 
Taarifa hiyo imeanza kutoa hali ya wasiwasi kuwa ligi huenda ikawa ngumu msimu huu kwa kuzingatia ukweli kuwa bado kuna hali ya sintofahamu juu ya mgawo wa pesa za mdhamini mtarajiwa ambaye ni Vodacom ambaye mpaka sasa bado anaendelea kutofautiana na pande nyingine husika kama vile Kamati ya ligi,  viongozi wa vilabu na hata TFF yenyewe.

Taarifa ya mapato ya michezo ya ufunguzi wa ligi imeonyesha wazi kuwa vilabu viwili vikubwa vikivuna mapato makubwa katika michezo yao na hali inaonekana kuendelea kuwa hivyo katika michezo yao yote kutokana na vilabu hivyo kuwa na mashabiki wengi hapa nchini. 
 
Mapato madogo ya michezo ya vilabu vidogo ni chagizo la kudumaa kwa soka la nchi yetu. Turudi kutazama upya kanuni na miongozo yetu ya mikataba ya wadhamini wa ligi ili kuviokoa vilabu hivi ambavyo havina mashabiki wengi ili viweze kutoa ushindani kwa vilabu vikubwa katika kila eneo ikiwa ni pamoja na suala zima la uchumi.
 
Kwa mtazamo wangu Afrikan Lyon imepiga hatua kubwa na ya kupongezwa katika kujitafutia mdhamini wake ambaye ni Zantel, hivyo tukarekebishe mikataba yetu na mdhamnini mkuu Vodacom licha ya kwamba wana biashara zinazo fanana.
 
Ukweli ubaki palepale tu kuwa udhamnini wa Vodacom ulihitajika kurekebishwa sana toka mapema kwa faida ya vilabu shiriki katika ligi na si kuvibana vilabu kwa misingi ya mfanano wa kibiashara hata kama fungu ni dogo.
 
Natumia mfano wa wadau wengi nchini ambao wamekuwa wakiutoa katika ligi kuu ya England kuwa licha ya kudhaminiwa na Backlays Bank, bado milango iko wazi kwa mabenki kudhamni vilabu.
 
Mantiki ya hili ni kuwa si rahisi Backlays  kuidhamini ligi na vilabu vyote 20 vya ligi hiyo na kuvitosheleza kila kitu kuanzia malazi, mazoezi na kambi, usafiri , programu za kimaendeleo , utawala na mambo mengine ya kiutendaji.
 
Tufike wakati tupiganie maendeleo ya kweli na dhamira ianze sasa na sio kesho,tusikubali kuyumbishwa na mitazamo hasi inayo akisi siasa katika mpira wa miguu na kuukimbia uweledi katika kuendesha soka.
 
Angalia mapato uwiano uko wapi

MAPATO YA MICHEZO YA JANA

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
 
Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
 
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
 
Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
 
112 WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING
Watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
 
Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
 
Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.

No comments:

Post a Comment