KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 16, 2012

Puyol nje wiki sita PUYOL NJE WIKI SITA.


Mlinzi wa Barcelona Carles Puyol anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya kuendelea kusumbuliwa majeraha ya mguu
Puyol mwenye umri wa miaka  34, alitolewa katika kipindi cha pili katika mchezo wa ushindi wa bao 4-1 dhidi Getafe na sasa anatarajiwa kuwa nje kwa karibu mwezi mzima.
Mlinzi huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vingine hii leo ambapo kocha wake Tito Vilanova anatarajia jiraha lake halitakuwa la muda mrefu.
"Puyol ni muhimu sana tunaimani atapona haraka, tumekuwa mara nyingi tunakabiliwa na majeraha katika sehemu yetu ya ulinzi wa kati "
Naye Gerard Pique akaongeza
"hali ya mambo sio nzuri kwasababu tuna wachezaji wengi wako nje, lakini tutakabiliana nalo."
Puyol alikosekana katika kikosi cha Hispania katika michuano ya Euro 2012 kutokana na kukabiliwa na tatizo hilo ambalo lilimpelekea kufanyiwa upasuaji.

No comments:

Post a Comment