KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 16, 2012

MAZEMBE HOI KWA BEREKUM CHELSEA SASA KUCHEZA NA WAARABU WA ESPERENCE.


TP Mazembe ya DR Congo imepoteza uongozi wa kundi la B katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika baada kukubali kufungwa bao 1-0 na Berekum Chelsea ya   Ghana mchezo uliofanyika hii leo nchini Ghana.
Bao pekee la washindi limepatikana kunako dakika ya 80 na mfungaji ni J. Opoku.
Nafasi ya uongozi wa kundi sasa inakamatwa na Al Ahly baada ya kwenda sare ya bao 1-1 na El Zamalek.
Zamalek walikuwa wa kwanza kupata kunako dakika ya  44 likifungwa na M. Ebrahim wakati ambapo bao la kusawazisha la Al Ahly likifungwa na M. Barakat.
Matokeo hayo sasa yana maanisha kuwa timu zote hizo Mazembe na Al Ahly zimefuzu hatua ya nusu fainali ambapo sasa watapambana na timu mbili za kutoka kundi A za Sunshine Stars na Esperance Tunis.

Nusu fainali
Al Ahly vs Sunshine
Esperernce vs Mazembe

No comments:

Post a Comment