KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 17, 2012

ANDY MURRY APELEKA MEDALI YA OLYMPIC NA TAJI LA US OPEN NYUMBANI ALIKOZALIWA NA KUPOKELEWA KAMA MFALME.


Andy Murray akusanya kijiji nyumbani Dunblane
Maelfu ya watu wamejitokeza katika mitaa ya kitongoji cha Dunblane alicho zaliwa bingwa wa mchezo wa tennis wa michuano ya wazi ya US Open na mshindi wa medali ya dhahabu ya michezo ya Olympic Andy Murray, kwa lengo la kumlaki na kumpongeza kwa ushindi aliopata.

Murray aliwasili katika mji huo wa nyumbani akiwa katika basi lililo wazi kabla ya kushuka na kuanza kutembea kwa miguu kwa lengo la kutia saini ‘autographs’ za mashabiki na kusheherekea nao kwa pamoja mafanikio aliyoyapata katika kipindi hiki cha kiushindani cha majira ya kiangazi.

Mkali huyo wa mchezo wa tennis amekaririwa akisema hiyo ilikuwa ni nafasi nzuri ya kukutana na marafiki, familia na jamii ya watu wanao mzunguka.
Mashabiki walikuwa wakiimba na kutaja jina la Murray baada ya kumsubiri kwa muda mrefu.

Mama yake na Murray Judy amesema ameshuhudia umati mkubwa wa watu wakimsubiri mwanawe
   “ilikuwa ni siku kubwa, kwa kweli nimefurahi sana kuwa sehemu ya tukio hilo”
Baada ya tukio hilo, Murray alinukuliwa na BBC Scotland akisema
"ilikuwa ni siku kubwa , nimefurahi sana. Nilikuwa na familia yangu yote na marafiki zangu wengi toka shule na waalimu ambao walinifundisha kila kitu, kocha wangu wa zamani wa tennis. Ilikuwa ni siku nzuri sana nimefurahi sana.
"hivi ni viwanja nilivyo anzia kucheza na kurejea hapa na kuona watoto wengi wamesimama juu yake, siamini macho yangu. Walikuwa wana kaa kimya wakiniangalia nikicheza hivyo kuwaona watoto wengi wamesimama na wanafurahia ni jambo zuri sana na nawataka waendelee hivyo."

No comments:

Post a Comment