KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 17, 2012

KIMATAIFA:MILITO ANASEMA USHINDI NI JUKUMU LA TIMU YAKE YA INTER, BUSQUETS ASHANGAA MATAJI BARCA NA FABREGAS ANAIOMBEA ARSENAL KUTWAA MATAJI.


Ushindi ni jukumu la Inter, anasema Milito baada ya ushindi dhidi ya Torino
Diego Milito amesema amefurahishwa na ushindi wa Inter wa mabao  2-0 dhidi ya Torino katika mfululizo wa michezo ya ligi ya Italia maarufu kama Serie A usiku wa jana na kusisitiza kuwa kwake hiyo ndio dhamira kubwa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alikuwa katika kiwango kizuri ambapo pia alifunga bao la uongozi mbali na kupiga pasi ya mwisho katika bao la pili la Nerazzurri ambapo amesema hafurahii mafaniko yake binafsi bali kwa timu nzima.
Amenukuliwa na Inter Channel akisema
"nimefurahi kufunga bao la kwanza na kuwa kinara katika mchezo . siku zote nimekuwa nikisema kitu muhimu ni kupata points tatu. Lakini kuingia katika orodha ya ufungaji ni jambo zuri pia"
Kocha mkuu Andrea Stramaccioni amesisistiza Milito ni mchezaji muhimu kwa Inter, na amekuwa akimpa moyo katika kikosi chake.
Milito amesha funga mabao mawili katika michezo mitatu ya mapema ya Serie A msimu huu.

Busquets: sikuwahi kufikiria kupata mataji mengi nikiwa na Barcelona
Sergio Busquets ametanabaisha kuwa mafanikio yake ndani ya Barcelona yamempa mshangao kwa kuwa hakuwahi kufikiria kuwa atakuwa mtu wa mafanikio na kuwa mchezaji muhimu katika klabu hiyo na kushinda mataji mengi
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 alianza kuitumikia Barca 2008,na tangu wakati huo amekuwa ni kiungo muhimu ambapo amefanikiwa kushinda mataji matatu ya ligi na mawili ya vilabu bingwa ulaya.
Amenukuliwa akisema katika mkutano na waandishi wa habari
"mambo haya yamekwenda haraka na ukweli ni kwamba sikuwahi kufikiri kushinda mataji mengi , ninafuraha sana kazi yangu imekuwa muhimu, nimecheza sana na sikuwahi kufikiri hivyot. Nategemea kuwa na miaka mingi na Barca na kushinda mataji mengi zaidi."

Wenger ataipeleka Arsenal katika changamoto ya mataji: Cesc Fabregas

Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amedai kuwa Arsene Wenger ana kipaji cha pekee cha kuendeleza vijana na amesisitiza kuwa kocha huyo Mfaransa ataanza kuzindua changamoto ya mataji Arsenal msimu huu.
Fabregas, ambaye aliondoka Arsenal August 2011, anaamini meneja huyo mwenue umri wa miaka 62 anauwezo wa kujenga hali ya kujiamini kwa vijana na kusema kuwa yeye licha ya kuondoka amekuwa akiifuatia mwenendo wa klabu yake hiyo ya zamani.
"Arsene Wenger ni mtu wa ajabu na nina uhakika atathibtisha hilo msimu huu. Siku zote anasaka vijana bora ulaya na huwapa moyo na kuwapa nafasi " Fabregas alikuwa akiongea na The Sun.
 "hicho ni kipaji chake cha kipekee ndivyo anavyo fanya kazi kuwapa moyo na kuwajenga kufanya kwa uwezo wao wote. Ndio maana nina uhakika Arsenal itakuwa katika changamoto ya mataji. Nawaangalia kila mwisho wa juma kwa kuwa Arsenal bado ina maana kubwa kwangu"

No comments:

Post a Comment