KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 9, 2012

MWANACHAMA WA YANGA AUWAWA MBEYA.


Mwanachama wa klabu ya Yanga Mzee Joseph Mwasokwa ameuwawa kikatili nyumbani kwake mkoani mbeya na watu wasiojulikana.


Kifo chake kimetokea wakati akirejea nyumbani usiku wa jana akitokea kuangalia soka barani Ulaya na alipofika nyumbani kwake alishambuliwa na watu wasiojulikana
Habari zaidi zinasema mzee huyo alikuwa kipenzi cha watu wengi anaishi nao karibu na nyumbani kwake  maeneo ya Block T.

Mwenyekiti wa mtaa wa block T mzee Adrian Maghembe ameshangazwa na mauji yake huku akisema wauwaji hao hawakuchukua kitu chochote cha marehemu zaidi ya kuitoa roho yake.

Kwa upande wake mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amewataka wananchi wa maeneo hayo na wote walioguswa na msiba huo kuwa na moyo wa subira wakati huu jeshi la polisi likifanya uchunguzi wa kifo chake na kuwasaka waliofanya unyama huo.

Marehemu Mwasikwa alikuwa mwanachama wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam mwenye kadi ya mwaka 2001 nambari 0361.
(Kutoka Mbeya yetu blog).

No comments:

Post a Comment