KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 10, 2012

AHSANTE SANA RAIS KIKWETE KWA NISHANI YA HESHIMA YA UTUMISHI NA UADILIFU WA BI KIDUDE NDANI YA TAIFA LA TANZANIA 'THANK YOU'

Fatuma bint Baraka a.k.a Bi Kidude akipokea nishani ya heshima kutoka kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete tuzo ambayo imetolewa siku ambayo Tanzania imetimiza miaka 51 ya uhuru.
 Historia fupi ya Bi Kidude.

Fatuma binti Baraka (aka Bi.Kidude) ni mwimbaji wa muziki wa Taarab toka visiwani Zanzibar. 

Anaangaliwa kama ni malkia wa muziki wa Taarab na Unyago nchini Tanzani, ambaye kipaji chake kiligunduliwa na kuimarishwa na mkongwe wa muziki wa aina hiyo kati ya miaka ya 1880 mpaka 1950, aliyejulikana kama Siti binti Saad.


Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, akiwa ni mtoto wa mfanyabiashara wa nazi enzi za ukoloni nchini Zanzibar.

Mpaka sasa watafiti wa mambo hawajui ni hasa tarehe ya kuzaliwa bibi huyu kwasababu sehemu kubwa ya historia zinazo husu historia ya maisha ya bi Kidude hazioani na hivyo na hivyo kuwepo na taarifa ambazo ni za kubuni.
Akiwa kwenye Tamasha la sauti za Busara Zanzibar.

Mwaka 2005 Bi Kidude alipewa tuzo ya heshima ya dunia WOMEX tuzo ambazo zilibuniwa mwaka 1999 na mbazo wanazawadiwa watu ambao wamepata mafanikio makubwa katika muziki au wametoa mchango mkubwa katika muziki, umuhimu wa mtu katika jamii na hata , mafanikio ya kibiashara na kwa upande wake ilitokana na mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar.


Akiwa mdogo alisifiwa sana kutokana na sauti yake na katika miaka ya 1920 alianza kuimba na vikundi mbalimbali vya kitamaduni.


Akiwa na umri wa miaka 13, baada ya kulazimishwa kuolewa aliamua kutoroaka na kuelekea Tanzania bara. 


Bi Kidude amezunguka Afrika mashariki yote akiimba taarab ambapo alitembelea miji mikubwa ya ukanda wa pwani pamoja na bara upande wa ziwa Victoria na Tanganyika. 


Mwaka 1930 alirejea Dar es Salaam na kujiunga na kikundi cha Egyptian Taarab ambacho alidumu nacho kwa miaka mingi. Katika miaka ya 1940 alirejea Zanzibar na kujenga nyumba yake iliyokuwa ya matope na kuanza maisha mapya hapo.


Alikuwa maarufu sana kwa shughuli za unyago ambazo ziliwaandaa masichana wadogo kuelekea katika ubalehe na kuingia katika maisha ya utu uzima.


Ni mtaalamu wa mambo hayo ya mila kongwe akifanya hivyo kwa wasichana akitumia mafunzo ya kitamaduni kuwaelekeza wasichana namna ya kuwapa raha waume zao na kuepuka migongano ya kifamilia na unyanyasaji wa mapenzi.
Hapa Bi Kidude katika Unyago

Sifa na jina la Bi Kidude lilikuwa na kusifika katika jamii yote ya Zanzibari na kuwa kielelezo cha utalii wa visiwa hivyo vya karafuu ambapo Hoteli mbalimbali kubwa na zenye hadhi ya juu visiwani humo zimekuwa zikizipa majina migahawa ya hoteli jina la Bi Kidude, mfano 236 Hurumzi inatumia jina la mgahawa wake jina la 'Kidude'.

No comments:

Post a Comment