KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 15, 2012

Mancini: Sheria za FIFA za kipumbavu


Meneja wa Manchester City Roberto Mancini kwa mara nyingine tena ameonyesha kushangazwa kwake na sheria za shirikisho la soka Duniani FIFA kufuatia hivi karibuni kuiitwa katika timu ya Taifa kwa mshambuliaji wake aliye majeruhi Sergio Aguero, na kuziita sheria za FIFA kuwa ni za kipumbavu.
Aguero amekuwa nje ya uwanja kufuatia maumivu ya mguu tangu mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa msimu wa ligi kuu ya England ‘Barclays Premier League’ ambao City walikuwa dimbani dhidi ya Southampton wiki nne zilizopita.

Lakini licha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutakiwa kuwa nje ya dimba mpaka mwishoni mwa juma hili, hilo halikumzuia kocha wa Argentina Alejandro Sabella kumwita katika kikosi chake kwa ajili ya michezo miwili ya kampeni ya kuwania kucheza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Paraguay na Peru.

Mancini amekubali kuwa kocha huyo alikuwa na haki ya kumwita kikosini lakini kwa kumfanyia uangalizi wa matibabu yake kwa mujibu sheria za bodi ya utawala ya fifa, lakini hawakuona hilo kama lingemsaidia na kumpa nafuu mchezaji huyo.

Alipoulizwa kama  Aguero amesalia katika klabu yake katika kipindi cha kufanyika michezo hiyo Mancini alijibu  “Hapana, meneja wake alimtaka, na atakuwa huko kwa siku tano, alifanyiwa uangalizi na wataalam, meneja alimtaka“.

“Hii ni sheria ya kipuuzi kwasababu , kama tuna mchezaji ambaye ni majeruhi kwa wiki mbili , ni vema akasalia hapa.”
Mancini ameielezea sheria hiyo kama ni sheria ya kuchekesha pale aliposikia kuwa Aguero ameitwa katika timu ya taifa, ambapo hapo kabla alitegemea kuwa mchezaji huyo angeruhusiwa kubakia England.
Pamoja na hilo, Aguero alitakiwa kufanyiwa kipimo cha afya yake leo kabla ya mchezo dhidi ya Stoke.
Mchezaji huyo aliyejiunga na City kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni £38, alianza mazoezi tena mapema wiki hii huku tayari kukiwa na matumaini ya kuwepo dimbani katika mchezo utakao pigwa Britannia.

No comments:

Post a Comment