Kiprotich Stephen |
Kwa kila mtanzania mpenda michezo siku ya leo ni msiba mkubwa katika michezo kufuatia kwa mara nyingine tena timu yetu ya Tanzania kupitia mchezo wa riadha tukimaliza michezo ya Olympic kule London Uingereza na kukosa medali.
Timu ya taifa ya Olypmic leo ilikuwa ikiwakilishwa na wanariadha wawili wa mbio ndefu(Marathon) Mussa Faustine na Samson Ramadhani ambao wote wameshindwa kufua dafu katika mbio hizo na kukamilisha michezo hiyo ambayo usiku wa leo itafungwa rasmi majira ya saa tatu usiku.
Usiku huu wa leo watakwenda kuyafunga rasmi na kesho jioni wamealikwa kwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza na kesho kutwa watakuwa wakirejea bila ya medali tukawapokee washujaa wetu hao kwa ngoma na vigelegele katika uwanja wa taifa wa ngege wa mwalimu Nyerere.
Mussa Faustine amekimbia mbio hizo na kukamata nafasi ya 33 akikimbia kwa kutumia muda 2:17:39 na Samson Ramadhani akishika nafasi ya 66 na kutumia muda wa 2:24:53
No comments:
Post a Comment