Mjumbe wa
kamati ya sheria na katiba ya shirikisho la kandanda nchini TFF Ismail Aden
Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Tanzania Simba, amaua
kujizulu kutoka katoka katika kamati hiyo ya tff kufuatia sakata la usajili wa
mlinzi wa APR ya Rwanda Mbuyi Twitte ambaye inaarifiwa kuwa amejiunga na klabu
ya Yanga.
Sambamba na
hilo pia Rage amefikia umauzi huo baada ya kubaini kuendelea kufanyika kwa madudu
na mchezo mchafu unaofanywa na sekretarieti ya TFF ambayo imekuwa ikisimamia
mambo bila kufuata kanuni na taratibu.
Akiongea na
Rockersports Rage amesema kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakiamuliwa kwa kukidhi
matakwa ya klabu Yanga hata kama ni kwa kuvunja sheria hasa panapo kuwepo na
‘conflict of interest’.
Rage amesema
mara mbili amemuandia barua Rais wa TFF Leordigar Tenga juu ya madudu hayo
lakini bado kumeendelea kujitokeza uvunjifu wa kanuni na sheria hasa katika
kamati ya maadili na katiba ambako yeye pia mjumbe.
Amesema mara
nyingi linapo jitokeza suala la kuijadili Simba ili kuruhusu haki kutendeka
amekuwa akitoka nje ili kutoa nafasi kwa suala hilo kujadiliwa kwa uwazi na
sheria kuchukua mkondo wake lakini hilo limekuwa halifanywi na viongozi wa
vilabu vingine hasa Yanga na maamuzi kuwa ni ya upendeleo.
Jambo
lingine Rage amesema ni kuridhika kwa Sekretarieti ya TFF juu ya mchezaji wake
mlinzi wa Kelvin Yondani kutolewa kambini usiku mwingi kwa lengo la kukamilisha
usajili katika klabu ya Yanga jambo ambalo amesema alimuandikia barua Rais Tenga
kumuarifu juu ya hilo lakini kabla ya hatua kuchukuliwa kamati ndogo ya sheria
ya TFF chini ya katibu wake Angetile Oseah iliamua kumuidhinisha Kelvin Yondani
kuchezea Yanga katika michuano ya kombe la Kagame.
Rage pia
amezungumzia juu ya usajili wa mlinzi wa kati wa APR ambaye kwasasa amesajiliwa
na Yanga amesema kuna mkono wa TFF kwani hilo limethibtishwa na Rais wa klabu
ya APR Meja Jenerali Alex Kagame pale alipozungumza naye juu ya taarifa za
mabadiliko ya usajili wake kwenda Yanga.
Amenukuliwa
Rage na Rockersports akisema
“wakati taarifa hizo zilipotufikia Simba niliamua kumpigia simu Rais wa APR Meja Jenerali Alex
Kagame ambaye alinithibtishia kuwa ni kweli klabu yake ilitoa ruhusa Simba
kumchukua Mbuyi na si Yanga, lakini kilicho fanyika ni kuwa amepewa maagizo na
wakubwa kumsainisha Twite katika klabu ya Yanga na hivyo taratibu za uhamisho
zikafanyika ili mchezaji huyo ajiunge na Yanga”.
“nikiendelea
kuzungumza naye alisema kuwa kuwa suala hilo limemfunga mikono kwani kuna
maagizo kutoka juu na kwamba kuna motto wa kigogo aliyekuwa ana shughulikia
suala hilo, hivyo lilikuwa juu ya uwezo wake”
Rage
amewashukuru wajumbe wote aliokuwa nao katika kamati hiyo kwa ushirikiano wao
na yeye ameamua kukaa pembeni lakini amemshukuru Rais Tenga kwa kumteu na kuwa
na imani naye katika kipindi chote alichukuwepo ndani ya kamati hiyo.
Rage
ameitahadharisha TFF na Serikali kuwa uvumilivu wa wanachama wa Simba utafika
mwisho na wasipokuwa makini watahatarisha amani ya nchi kwani huko nchini Kenya hivi karibuni timu ya Abaluya na Gor Mahia wapenzi wao
waliuana kwa mambo kama hayo ya michezo, hivyo tunapaswa kuwa makini.
Simba na Rage kilichobaki ni kuendelea kulia tu ...
ReplyDelete