Fifa yaanza tena kumchunguza Mohamed
bin Hammam
Mohamed Bin Hammam |
Bodi ya
utawala ya shirikisho la soka duniani fifa imeanza tena kumchunguza Rais wa
zamani wa shirikisho la soka barani Asia Mohammed Bin Hamman juu ya uvunjifu wa
sheria za shirikisho hilo
Qatari ilifungiwa
kutokujishulisha na mambo ya soka kwa siku 90 kuanzia July 26 2012 baada ya
kuonekana kufanya vitendo vilivyo fanana na rushwa katika mpango wao wa kusaka
nafasi ya Urais wa Fifa mwaka 2010.
Hapo kabla
Bin Hammam alipewa adhabu ya kutokujishulisha na soka maisha kabla ya adhabu
hiyo kutengeliwa na mahakama ya usuluhishi ya michezo CAS July 19 kufuatia
kukosekana ushahidi uliojitosheleza.
Bin Hammam alikuwa
ni mpinzani mkubwa wa Sepp Blatter katika kampeni za urais wa fifa na alikuwa
akifanya kampeni ya gharama kubwa kumng’oa Baltter akitumia ndege binafsi
lakini baadaye katuhumiwa kufanya kampeni chafu.
Di Matteo anasema Manchester City & United wako mbele zaidi
ya Chelsea licha ya matumizi makubwa ya usajili kiangazi.
Roberto Di Matteo |
Meneja wa Chelsea
Roberto Di Matteo amekubali kuwa timu ambazo zimekuwa zikionekana kwenye nafasi
ya kutwaa taji msimu ujao wa ligi ya uingereza Manchester City na Manchester
United bado ziko mbele ya Chelsea licha ya ‘the Blues’ kufanya usajili kwa
mapesa mengi.
Mtaliano
huyo ameweka wazi kuwa viungo washambuliaji Eden Hazard, Marko Marin na Oscar katika
kikosi chake msimu huu wameigharimu klabu yake pauni milioni £65.
Chelsea inatarajia
kucheza katika mchezo wa ngao ya jamii “Community Shield” jumapili hii dhidi ya
Manchester City na Di Matteo ametabiri kuwa watadhihirisha kuwa wako vizuri.
"Manchester
City ni mabingwa wa msimu uliopita, lakini tutawafunga hata kama United ndiyo
inayoonekana kuwa nyuma yao kiubora.
Wakati
Chelsea ikielekea katika ufunguzi wa pazi la ligi kuu ya Uingereza, pia klabu
hiyo itakuwa ikiingia katika msimu mpya wa kimashindano katika michuano ya Uefa
Super Cup na Fifa Club World Cup ikiwa ni kufuatia kupata mataji ya FA Cup na
klabu bingwa.
Di Matteo anasema
wanapaswa kupigania mataji mengine lakini kikosi chake kuongeza jitihada katika
ligi kuu msimu kufuatia kumaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita 2011-12.
Manchester United itaendelea kuwekeza
kwa wachezaji anasema mtendaji mkuu David Gill
Mtendaji
mkuu wa Manchester United David Gill amewatetea wamilikiwa klabu hiyo na
kusisitiza kuwa wanaelewa umuhimu wa kuendelea kuwekeza katika wachezaji.
Gill amesema
hayo kufuatia United kuweka sokoni hisa zake katika soko la New York Stock
Exchange kujaribu kupata pesa zaidi ili kupunguza deni linalo ongezea Old
Trafford.
Licha ya
kwamba hilo bado halija fanikiwa kama United inavyo tumainia , Gill amesisistiza
kuwa mfumo wa kifedha uliopo kartika klabu hiyo unaonyesha kuwa klabu hiyo
itaendelea kutumia pesa zake katika kuimarisha kikosi.
Amenukuliwa akisema
"tunafahamu
na wamiliki wanaelewa kuwa kinachotokea uwanjani ni muhimu sana kwetu na tutafanya
kila linalowezekana pesa inatumika kuwekeza katika timu ili tusonge mbele".
akizungumzia wamiliki wa Glazer family amesema
"ukubwa
wa deni tulilo ingia huko nyuma tangu wachukue klabu halina madhara kwa timu” .
Mtendaji huo
ameendelea kusema kuwa mafanikio ya klabu hiyo katika Premier League na Champions
League pamoja na makubaliano ya udhamini wa jezi na na kampuni ya Chevrolet ni
katika jitihada za kuendeleza kutafuta pesa bila kujali deni la klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment