Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage |
Myenyekiti
wa klabu ya soka Simba Ismail Aden Rage amesema amesikitishwa na kitendo
kilicho fanywa na mahasimu wao katika soka Yanga kwenda kumsajili mlinzi wa
Kati wa klabu ya APR ya Rwanda Mbuyi Twite kinyume na taratibu za kisoka.
Akiongea na
Rockersports Rage amesema kitendo hicho ni sawa na unyama na si uungwana kwani
tayari walikwisha kumalizana na mchezaji huyo lakini kitendo kilicho fanywa na
Yanga kwa kushirikiana na shirikisho la
soka nchini Tanzania TFF si uungwana.
Rage amesema
wao kama Simba tayari walimpatia Mbuyi Twite dola elfu 30 kwa mkataba wa miaka miwili na kimsingi
walikubaliana naye mbele ya Rais wa klabu ya APR Meja Jenerali Alex Kagame.
Lakini wakati
Simba wakidhani wamesha yamaliza na wakiwa wanamsubiri Mbuyi Twitte kutua Msimbazi
ndipo mambo yalipo badilika na taarifa kuifikia Simba kuwa mchezaji huyo amesajili
wa wapinzani wao Yanga.
Rage amesema
kilicho fanywa na Yanga wakishirikiana na TFF ni kutumia wakubwa na hasa
akimtaja mtoto wa Kigogo ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake ambaye naye aliwatumia wakubwa wa Rwanda kukamilisha
usajili wa Mbuyi Twite ambaye kwasasa anawasubiri Yanga ambao wana ratiba ya
kwenda kuweka akambi nchini Rwanda.
Rage amesema
wakati taarifa hizo zikiwa zimewafikia Simba aliamua kumpigia simu Rais wa APR Meja
Jenerali Alex Kagame ambaye alimthibtishia kuwa ni kweli klabu yake ilitoa
ruhusa Simba kumchukua Mbuyi na si Yanga lakini kilicho fanyika ni kuwa amepewa
maagizo na wakubwa kumsainisha Twite katika klabu ya Yanga na hivyo taratibu za
uhamisho zikafanyika ili mchezaji huyo ajiunge na Yanga.
Rage amesema
hilo limemsikitisha yeye na uongozi wote wa Simba na kuwataka wanachama na
wapenzi wa Simba wawe watulivu kwa mamba hayo yana mwisho.
Kwasasa Rage
amesema wao kama Simba wamekubali yaishe isipokuwa wanaomba mchezaji huyo
kurudisha pesa alizochukua baada ya makubaliano na Simba ikiwa ni pamoja na
dola elfu 30,000 za usajili wake, gharama za usafiri wa kwenda Kigali mpaka
Lubumbashi na kisha kurejea Dar es salaam na hoteli, pamoja na gharama za
kuwalipa mawakili waliosimamia zoezi la usajili wake kisheria ambazo kwa ujumla
wake ni kiasi wa dolari za kiamrekani 9,000.
Rage amesema
hilo likishindikana watalazimika kupeleka mashtaka shirikisho la soka duniani
fifa kutokana na kitendo cha kitapeli kilicho fanywa na mchezaji huyo
kujisajili vilabu viwili.
No comments:
Post a Comment