Craig Bellamy |
Cardiff City
imetangaza kumsainisha mshambuliaji wa Liverpool Craig Bellamy kwa mkataba wa miaka
miwili.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Weles mwenye umri wa miaka 33 ambaye alitumikia msimu wa 2010-11
kwa mkopo kwa ‘ndege hao wa bluu’ amekamilisha vipimo vya afya huko South Wales hapo jana.
Bellamy amezaliwa
huko Cardiff ameamua kuachana na ligi kuu ya Uingereza na kushuka katika ligi
ndogo ya nyumbani kwao alikozaliwa na sasa atakuwa akivalia jezi nambari 39.
Msimu
uliopita ameicheza Liverpool jumla ya michezo 33 katika michuano mbalimbali
akifunga jumla ya mabao tisa.
Bellamy
anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake katika timu yake mpya kuelekea katika
mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Huddersfield Town.
No comments:
Post a Comment