Alou Diara |
West Ham imekamilisha
zoezi la kumsajili kiungo wa Marseille Alou Diarra kwa mkataba ambao ada ya
uhamisho haujawekwa wazi.
Kiungo huyo
wa kimataifa wa Ufaransa amekubali kuingia mkataba wa miaka miatatu ndani ya Upton
Park, na anakuwa ni mchezaji nane kusajiliwa na meneja Sam Allardyce katika
msimu huu wa uhamisho wa kiangazi.
Diarra ameichezea
Ufaransa jumla ya michezo 44 lakini pia akicheza michezo mitatu katika Euro
2012 ikiwa ni pamoja na mchezo wa ufunguzi dhidi ya Uingereza .
akiongea
kupitia mtandao wa klabu yake mpya ya West Ham Diara amesema
“nimefurahishwa
na kuwepo West Ham kila kitu kimesha sainiwa kitu ambacho ni kizuri na
nimefurashwa mno kuwepo hapa nikicheza katika ligi ya uingereza ‘Premier League”.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Bayern Munich akitokea Louhans-Cuiseaux
mwaka 2000 licha ya kushindwa kuichezea klabu hiyo ya Ujerumnai katika cha
kwanza.
Baadaye
alihamia Liverpool lakini kwa mara nyingine tena akashindwa kukichezea kikosi
cha kwanza na kuelekea nchini Ufaransa ambako ameendelea kucheza soka mpaka
sasa.
Baada ya
kujiunga na Lens mwaka 2005 kwa mkopo, Diarra akaelekea katika vilabu vya Lyon na Bordeaux kabla ya kujiunga na Marseille.
No comments:
Post a Comment