Shirkisho la
soka nchini TFF limeongeza muda wa usajili mpaka kufikia tarehe 15 saa jioni
ambapo pia imevitaka vilabu vyote kuhakikisha vinakamilisha zoezi hilo mpaka
kufikia siku hiyo.
Sambamba na
hilo shirikisho limevitaka pia vilabu hivyo kuwasilisha na majina ya wachezaji
wa timu zao za vijana wa under 20.
Kufuatia hali hiyo TFF pia imesogeza mbele muda wa
mapingamizi ya usajili na kamati ya usajili ikitarajiwa kukutana
tarehe 22 na 23 kupitia usajili huo.
Katibu wa
TFF Angetile Oseah amesema vilabu vya ligi kuu vinapaswa kuwasilisha majina ya
viwanja vitakavyo tumiwa na vilabu hivyo ikiwa ni pamoja na majina ya benchi
zima la ufundi wakiwemo makocha wa timu hizo.
No comments:
Post a Comment