Rais wa tff Sir Leordigar Chilla Tenga |
Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kuanza chini ya usimamizi wa chombo huru yaani kampuni, kuna kila dalili ya ligi hiyo kusogezwa mbele kutokana na ukweli kuwa mambo kadhaa bado hayajafikiwa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa chombo kitakacho simamia ligi hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Rais wa shirikisho la soka hapa nchini Leordiga Chila Tenga wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tff mwezi April mwaka huu alisema ligi ya mwaka huu itaendeshwa na chombo kingine tofauti na kamati ya ligi ya tff ambacho kwa utafiti wa Rockesports chombo hicho bado hakijaundwa.
Akiongea na Rockersports mwenyekiti wa kamati ya ligi ya ligi ya tff Wallece Karia amesema kamati yake bado inaendelea kusimamia mambo kadhaa ya kuanza kwa ligi hiyo licha utendaji ya tff iliyokutana wiki mbili zilizopita tayari kuidhinisha ligi hiyo kusimamiwa na vilabu vyenyewe, lakini bado structure kamili ya uongozi wa vilabu haijajipanga sawasawa kusimamia ligi hiyo msimu huu.
Wallace amesema kimsingi kamati yake ya ligi itakuwa inakoma kufanya kazi ya kusimamia ligi hiyo baada ya uzinduzi wa chombo hicho ambacho bado hakijaeleweka.
Rais wa tff Leordigar Tenga anatarajiwa kuzindua chombo hicho mapema kabla ya ligi kuanza huku mambo kadhaa ikiwemo muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili na kusikilizwa kwa mapingamizi haujafikia mwisho.
Yapo mambo kadhaa ambayo yanapaswa kukamilishwa kabla ya ligi hiyo kuanza ambapo kwasasa ndiyo kwanza tff na kamati ya ligi ya sasa kwa kushirikiana na viongozi wa vilabu wako katika mazungumzo na madhamni wa ligi hiyo kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Mambo mengine ni mtihani wa waamuzi yaani Copa test, pamoja na uthibitisho wa viwanja gani vitatumiwa na vilabu shiriki katika ligi hiyo mambo ambayo unaweza kuona kama ni madogo lakini yanahitaji muda na mazungumzo na makubaliano baina ya pande zote husika.
Wallece Karia amesema bado kamati yake inaendelea na mchakato wa kuelekea kuanza kwa ligi hiyo kwa kushirikiana na secretarieti ya tff pamoja na viongozi wa vilabu ili kukamilisha taratibu zote muhimu za kuanza kwa ligi hiyo ikiwemo suala la mdhamini Vodacom ambaye muda wa mkataba wa sasa wa Vodacom kuelekea kufikia ukingoni August 31.
MSIKILIZE WALLACE KARIA
MSIKILIZE WALLACE KARIA
Mwezi April Rais Tenga mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa tff alisema lazima katika msimu wa ligi wa 2012/2013 ligi hiyo itakuwa ikisimamiwa na chombo huru ambacho kitakuwa na majukumu ya kuendesha na kusimamia ligi ikiwa ni pamoja na suala la ratiba na kusimamaia adhabu.
Suala lingine ni usimamiaji wa mapato pamoja na kutengeneza management kwa kuajiri watendaji wakuu na kuajiri mhasibu wao jambo ambalo mpaka sasa hakuna dalili za watendaji hao kuwa tayari wameshaandaliwa.
SIKILIZA TENGA ALIVYOSEMA MWEZI APRIL
No comments:
Post a Comment