Jose
Mourinho anaamini sasa ataitwa the “Only one” badala ya the “Special One”,baada
ya kuwa kufanikiwa kuwa kocha pekee kushinda mataji matatu makubwa barani ulaya.
Akiongea na kituo
kimoja cha luninga nchini Ureno SIC hapo jana , Mourinho ameeleza kuwa kazi
yake ya umeneja imempa tabia nyingine kabisa ya kupunguza ubinafsi na kutokuwa
mtu mwenye mtazamo binafsi tena.
Amenukuliwa akisema
"mambo
yamekuwa yakienda vizuri kwa upande wangu namshukuru mungu amenipa kituo .
"
Nimekuwa ni
mtu nianye angalia wengine zaidi siku hizi. Furaha ya kushinda nilipokuwa na Inter
Milan ilikuwa ilionekana ya klabu ambayo haikushinda kwa miaka 50.
Mourinho alishinda
taji la ligi kuu ya soka nchini Hispania msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Real
Madrid, lakini huko nyuma alishinda mara mbili taji la ligi ya Italia Serie A akiwa
na Inter Milan.
Akiwa na Chelsea
alishinda taji la ligi kuu ya Uingereza ‘Premier League’ lakini kama hiyo
haitoshi akiwa na Porto alifanikiwa kushinda mara mbili taji la ligi kuu ya
Ureno ‘Portuguese Liga’. Zaidi ya hapo ameshinda vilabu bingwa akiwa na Porto na
Inter.
Amenukuliwa akisema
"kwangu
mimi ndiye mtu pekee kushinda mataji ya ligi kubwa na mashindano makubwa muhimu.
Hivyo pengine badala ya kuitwa The 'Special One', watu inabidi waanze kuniita The
'Only One',"
Bosi huyo wa
sasa wa Real Madrid alipewa jina la utani la “The Special One” akiwa nchini Uingereza
akiongea na waandishi wa habari mwaka 2004 akihamia Chelsea akitokea Porto ya
Ureno.
August 25 Real
Madrid itaumana dhidi ya wapinzani wao wakubwa Barcelona katika mchezo wa kuashiria kuanza
kwa ligi mchezo wa Spanish Super Cup.
No comments:
Post a Comment